BatteryLow
JF-Expert Member
- Aug 14, 2011
- 446
- 149
Habari wana jf. Naomba kueleweshwa hii kitu nasikia mwanafunzi amepewa mkopo wa elimu ya juu 54%. Ni kwamba Bodi itamalizia hiyo 46% baadae au ni mwanafunzi atalipa mwenyewe? Kama ni mwanafunzi atalipa mwenyewe baada yakusoma kwa kiwango cha hiyo 54% na akashindwa kumalizia 46%, nadhani maana yake ni kwamba hataendelea tena na masomo. Na lengo la huo mkopo ni kwamba mlengwa asome amalize na aajiriwe halafu alipe kidogo kidogo kwa kukatwa kutoka kwenye mshahara wake. Swali langu ndo liko hapo: Huyo mwanafunzi kalipiwa nusu na akashindwa kulipa iliyobaki na hakuweza kumaliza chuo, hivyo hatapata ajira ambayo inapelekea kushindwa kurudisha ile sehemu ya mkopo aliopewa. Je, maana yake ni kwamba Bodi wamepata hasara kulipia wanafunzi 1/2 ada halafu wakashindwa kuendelea, kwa vile pesa haitarudi? Au wanachukulia kwamba wote waliolipiwa nusu wana uwezo wa kumalizia sehemu iliyobaki?