Mwanafunzi anapopewa nusu mkopo

Mwanafunzi anapopewa nusu mkopo

BatteryLow

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2011
Posts
446
Reaction score
149
Habari wana jf. Naomba kueleweshwa hii kitu nasikia mwanafunzi amepewa mkopo wa elimu ya juu 54%. Ni kwamba Bodi itamalizia hiyo 46% baadae au ni mwanafunzi atalipa mwenyewe? Kama ni mwanafunzi atalipa mwenyewe baada yakusoma kwa kiwango cha hiyo 54% na akashindwa kumalizia 46%, nadhani maana yake ni kwamba hataendelea tena na masomo. Na lengo la huo mkopo ni kwamba mlengwa asome amalize na aajiriwe halafu alipe kidogo kidogo kwa kukatwa kutoka kwenye mshahara wake. Swali langu ndo liko hapo: Huyo mwanafunzi kalipiwa nusu na akashindwa kulipa iliyobaki na hakuweza kumaliza chuo, hivyo hatapata ajira ambayo inapelekea kushindwa kurudisha ile sehemu ya mkopo aliopewa. Je, maana yake ni kwamba Bodi wamepata hasara kulipia wanafunzi 1/2 ada halafu wakashindwa kuendelea, kwa vile pesa haitarudi? Au wanachukulia kwamba wote waliolipiwa nusu wana uwezo wa kumalizia sehemu iliyobaki?
 
Shukuru na hicho ulichopata, wengine wamekosa kabisa na wanaiomba bodi wawape hata nusu.
 
unajiita mgonjwa,ngoja uwaone wagonjwa wenyewe upone bila dawa,Nenda bodi kesho ujionee mtu yatima na one o level na advance lkn kaambulia nothing,,,,,,,
 
Shukuru na hicho ulichopata, wengine wamekosa kabisa na wanaiomba bodi wawape hata nusu.
Sawa hiyo tunaelewa tunashukuru kwa kidogo tulichopata, siyo kwamba ninalaumu mkopo kutolewa 1/2, ninachotaka kujua ni kwamba mwanafunzi anaposhindwa kumalizia sehemu iliyobaki, hiyo si hasara kwa Bodi? Maana yake hiyo pesa hairudi tena?
 
Nenda upitie tena vifungu vya heslb tena, wanasema ukishindwa kuendelea na mwaka mwingine eiza ulifeli mkopo utasitishwa
 
wengine hatuna hata chochote. 54% bado unalalamika !!!! hakika dunia haiko sawa
 
Back
Top Bottom