Mwanafunzi anatakiwa kuwa na simu darasa la ngapi?

Mwanafunzi anatakiwa kuwa na simu darasa la ngapi?

Nimemiliki simu nikiwa primary sababu ya kuwasiliana na wazazi manake hawakuwa wakaaji sana nyumbani....hata hivyo ilichukuliwa baada ya kuunga zile simu za mezani za TTCL
 
Kwa ujumla mwanafunzi anaeitwa mtoto (primary na secondary regardless O level or Adv) hatakiwi kumiliki simu mahali popte whether nyumbani au shuleni. Mzazi/mtu mzima tu ndiye mwenye haki ya kumiliki simu sababu hata usajili wa line ni kwa jina lake.

Kisheria, mtu yeyote haruhusiwi kutumia line ya simu ambayo haijasajiliwa kwa jina lake, bila kujali ni mtoto wako, mkeo, mumeo, ndugu, nk.

Tunaposema KUMILIKI SIMU ni tofauti na KUWASILIANA kwa SIMU. KUMILIKI SIMU maana yake ana full mandate ya kui control na kutumia kadri ya mapenzi yake yatakavyomsukuma bila kusahau uwezo wa kuihudumia km kuweka vocha na maintainance.

KUWASILIANA kwa SIMU maana yake ni kutumia kifaa hicho km chombo cha kupashana habari/taatifa regardless the age of communicators. Hapa ndo utaona mzazi/mlezi ana nunua SIMU ya mezani ili kuwasiliana na mfanyakazi wa ndani au watoto wake pindi wanapokuwa nyumbani kwa ajili ya emergency cases. Hapa mzazi/mlezi anakuwa na full mandate ya kui control ikiwa ni pamoja na kuweka vocha na maintainance.

Hivyo, KUWASILIANA kwa SIMU hakuna boundary, mtu yeyote anaweza kufanya hivyo hata mtoto ambae hajaanza nursery ingawa nao hawataikiwi kutumia kwa muda mrefu sababu za kiafya. Inashauriwa wawekewe loudspeaker.

Kwa maelezo hayo hapo juu wewe unaeshaabikia mtoto KUMILIKI SIMU jihoji upo sahihi au ni kufuata mkumbo wa maisha ya kizungu. Km ni kuwaonesha upendo kuna namna nyingi za kufanya kuliko kumjengea upendo wa kumharibu. Na kwa nini sasa hamuwanunulii SMART PHONE, mnawanunulia VISWASWADU tu ha ha ha ha ha.

Kwa utafiti wangu mdogo ktk matumizi ya sm nimebaini yafuatayo:
1) Kwa watoto wadogo (under 18 yrs age including na wanafunzi wa msingi na secondary) 99% hutumia simu kwa mambo ya hovyo hovyo ikiwa ni pamoja na kuzitumia kwa ajili ya mawasiliano ya kimapenzi tofauti na wengi wanavyodhania na kushaabikia kuwa wanapaswa KUMILIKI SIMU. Ni 1% moja tu ndiyo hutumia kwa manufaa km kujisomea na kuwasiliana na ndugu na marafiki.

Mbaya zaidi uendeshaji wa SIMU hizo km kununua vocha na maintainance kwa 75% kunategemea kupata fedha kwa wanaume (boyfriends). Ni 25% tu wanaoomba pesa kutoka kwa wazazi/walezi wao. Hivyo SIMU kwa watoto kimekuwa chanzo cha kujihusisha na mapenzi ktk umri mdogo.
2) Kwa watu wazima 25% tu ndiyo hutumia SIMU kwa manufaa ya kujiingizia kipato, huku 75% hutumia SIMU kwa mambo ya hovyo hovyo km kuchart na wanaume/wanawake, kuangalia picha na video za ngono, kuingia fb, TikTok, Snapchat, nk kwa malengo ya kutafuta UDAKU huku wao wakichukulia km sehemu ya kupotezea muda na kujifariji.

Mwisho, watu tusipende kuiga maisha ya kizungu ambayo hayana faida yoyote kwa watoto wetu kwa kisingizio cha sayansi na teknolojia. Tutawaumiza na kuwspoteza ktk ulimwengu wa maadili.

NB
Kila mtu alee mtoto wake kadri anavyoona ni sahihi, maneno yangu siyo msaafu.

Nimemaliza: BANDOKITITA
 
Back
Top Bottom