Mwanafunzi anayedaiwa kuchapwa viboko na kumuacha na uvimbe na makovu Dodoma

Mwanafunzi anayedaiwa kuchapwa viboko na kumuacha na uvimbe na makovu Dodoma

Vitoto vya siku hizi vina viburi na maadili ni sifuri, nao walimu hawana maadili, wazazi nao ni wa ovyo , yaani tafrani tu .

Nilishapigwa fimbo kama 90 , mzazi kuniona nimevimba akanichukua akanirudisha shule walimu wakampa maelezo , kengele ikapigwa mzee akanikaragaza fimbo kama utitiri pale paredi.
 
Tatizo la walimu wanajilimbikizia madeni mengi kiasi cha kuwa na stress na chuki na kazi zao.

Ukute teacher kapokea salary slip yake ina laki moja to kutoka milioni 1 ya mshahara , nyingine yote imefyekwa na makato ya mikopo toka sehemu mbali mbali.

Ila naomba Mungu aniepushie jambo kama hili kutokea kwa mwanangu maana nina hakika segerea itanihusu.
 
Vitoto vya siku hizi vina viburi na maadili ni sifuri, nao walimu hawana maadili, wazazi nao ni wa ovyo , yaani tafrani tu .

Nilishapigwa fimbo kama 90 , mzazi kuniona nimevimba akanichukua akanirudisha shule walimu wakampa maelezo , kengele ikapigwa mzee akanikaragaza fimbo kama utitiri pale paredi.
Wewe unafikiri hiyo ilikusaidia?

Kumpiga sana mtoto kunamfanya awe sugu tu.

Mtoto akifanya kosa sio lazima upige kama nyoka, unaweza kumpa adhabu nyingine yenye faida, na akajifunza akabadilika.
 
Wewe unafikiri hiyo ilikusaidia?

Kumpiga sana mtoto kunamfanya awe sugu tu.

Mtoto akifanya kosa sio lazima upige kama nyoka, unaweza kumpa adhabu nyingine yenye faida, na akajifunza akabadilika.
Ni kwel unachokisema kwa sasa ,ila kwa kipindi hicho tulipigwa vibaya mno na kwa hilo tulijifunza kuchapa kazi na kuvumilia katika kila hali , ila nakuunga mkono hoja yako.
 
Kuna mwalimu mmoja alimpiga mwanafunzi viboko 99, mwanafunzi alikuwa wa kiume baada ya kuchapwa alivimba makalio akawa ana msambwanda,

wazazi wa mwanafunzi wakaenda polisi badae hospitali mwanafunzi alikuwa hawezi kukaa, kesi ikaanza.

mwalimu kuulizwa amechapa viboko vingapi anasema yeye amechapa kiboko kimoja. kweli daktali baada ya kumtibia akasema mwanafunzi amechapwa kiboko kimoja.

kumbe yule mwalimu alikuwa anapiga palepale.
 
Mimi nakubali sana wale walimu wenye msimamo wa 'Sigusi mtoto wa mtu, atajijua na mzazi wake'.
Hii nayo siyo nzuri.

Ni kama anawasusa watoto.

Toa adhabu moderate tu kwa mtoto, ukiona anaendelea kufanya makosa, kupiga sana siyo solution.

Ni lazima kwanza mjue kwa nini anabehave hivyo, mara nyingi ni mazingira(situations or certain conditions).

Kumsaidia ni kutatua hizo conditions.

Unawekuta mtoto anachelewa kila siku, kumbe anakaa na mama wa kambo, akiamka asubuhi anaambiwa afanye kazi kwanza ndio aende shule.

Na nyie mmeng'ang'ana kupiga tu.
 
Kuepusha kumshikia mwalimu glock ya kichwa bora uamishe mtoto wako shule tu peleka private maana walimu wa serikalini wana stress za mishahara na kikotoo nacho kinawalima makato marefu mno, wamebaki wanapiganiana mikakati na mitihani isiyoisha ili wapate nyongeza angalau wasukume maisha .

Immagine mwalimu anatuma mtoto akavunje bulb ya darasani ili kesho akija achangishe darasa zima apate angalau 30k ya kufungia siku soo sad.
 
TZ hadi umalize kusoma una makovu mengi sana na chukiii. Makovu mwilini na rohoniii .... Yalosababishwa na wanafunzi wenzio ama waalimu
 
Back
Top Bottom