Watoto wa Kitanzania wamelelewa katika nidhamu ya woga. Mtoto muda wote ana hofu atakosea ataadhabiwa. Hata kujieleza vizuri hawezi sababu ya woga.
Mnasema fimbo ni kwa ajili ya kunyosha maadili lakini ni nani anaangoza kwa kuwa na maadili ya hovyo kati yetu na Wazungu?
Nani anayeua Albino?, nani mla rushwa?, nani fisadi?, nani anaibia majeruhi wa ajali?, nani wanaopitisha miswada ya kukandamiza watu wao?
Hii dhana ya Kitanzania manguvu mengi akili kidogo inaturudisha nyuma sana. Kila sehemu tunaamini nguvu ndio suluhisho. Mtu kamsaidia binadamu mwenzake aliyepatwa na ajali, kamfikisha Polisi apate Pf3 akatibiwe cha ajabu anawekwa ndani yeye ndio kamgonga.
MANGUVU MENGI AKILI KIDOGO, MATOKEO MADOGO.