Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 620
- 1,240
Mwanafunzi mmoja toka chuo cha Koteti Mkoa Tanga nchini Tanzania anaitwa Bonus Mbono nwenye umri wa miaka 21, amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu na kusomewa mashtaka matatu ikiwemo kuchapisha taarifa za Uongo kupitia Mitandao ya kijamii TikTok.
Pamoja na kutumia line ya simu iliyosajiliwa kwa jina la Mtu mwingine. Mshtakiwa huuo alifikishwa mahakamani hapo Jumatatu, Machi 10, 2025 kwa ajili ya kusomewa Kesi ya Uhujumu Uchumi Namba 5907 ya mwaka 2025.
Mashtaka hayo yaliwasilishwa na Wakili wa Serikali Erick Kamala mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Gwantwa Mwankuga.
๐จ Kosa la kwanza ni kuhusu video iliyokuwa inasambaa mtandaoni kwenye mtandao wa TikTok ikimuonyesha Mwalimu Julius Nyerere akiwa anachezesha kichwa chake kwa kukitoa nje ndani kwenye Noti ya shilingi Elfu Moja ya Kitanzania video hiyo iliundwa kupitia Teknolojia ya AI.
๐จ Shitaka la pili linasema kupitia tarehe hiyo hiyo katika Eneo lisilojulikana , mshtakiwa alitumia kifaa kisicho halali kiitwacho Pix Vase kuunda na kupakia chapisho la uwongo kwenye TikTok, akijua kabisa kuwa ni kosa kisheria.
Shtaka la tatu linadaiwa Februari 10, 2025 katika Chuo cha Koteti jijini Tanga, Mbono alitumia SIM kadi iliyosajiliwa kwa jina la Prisca Anthony, kinyume cha sheria na bila kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Tujihadhari tunapotumia Mitandao ya kijamii โ