Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

Binti nawapa simu mwenyewe, akipata mimba nitalea mjukuu, akipata UKIMWI atameza ARV. Ila simu, computer, gari, exposure, life skills na Hofu ya MUNGU anavipata kutoka kwangu baba yake na mama yake, hayo ya HIV na Mimba naamini atayashinda.
@22 ruksa kuolewa. Before 22 yupo busy na biashara za familia, elimu kuanzia form 1 mpaka degree ni ndani ya mji ambao mm na mama yake tupo ili kumpa elimu ya maisha na biashara na uzoefu except kwa aliyechagua sayansi, huyo hata nje MUNGU akiruhusu ataenda.

Mambo ya mtoto yupo bording anatandikwa viboko 20 kumpa displine mm siyataki, usugu tu anatengenezewa na maisha yanahitaji experience sio usugu na ununda.
 
Yaani genge la watu ishirini wamesimama wima kukashambulia katoto ka kike!!

Hawa watu hawako sawa.
 
Huyo kahaba mmetoa huko kumuweka bweni ili atulie lakini bado anasumbua walimu na matron! Alafu mzazi unalalamika kwa walimu kwa uzembe na malezi yako mabovu.

Walimu Jangwano fukuzeni shule huyo changu asije haribu wengine humo bwenini.
 
Kuna waalimu, na askari ni makundi ya watu wajinga wanaotumia mabavu badala ya akili.

Kwanini usiwe mwalimu ili utumie akili zako nzuri?

Kwanini usiwe askari ili utumie akili zako nzuri?

Mwisho wa siku watu wote mnatetea walimu na mnaotete mwanafunzi hakuna mjualo zaidi ya mihemko tu maana hapa mmesoma uzi wa upande mmoja hamjasikiliza upande wa pili wa stori ili mpate uhalisia.

Huwezi kumhukumu mtu bila kusikiliza pande zote
 
Wewe hata mtoto huna!
 
Wewe ni mpuuzi na huenda ndo huyo mwanafunzi mwenyewe. Fimbo 20 kidogo kwa katoto ka F.3 kukutwa ama kuhisiwa kuwa na simu.
 
Wewe ni mpuuzi na huenda ndo huyo mwanafunzi mwenyewe. Fimbo 20 kidogo kwa katoto ka F.3 kukutwa ama kuhisiwa kuwa na simu.
By-laws za shule zinasema mwanafunzi akikamatwa na simu afukuzwe shule, SIO KUPIGWA MARUNGU.

Serikali ikiwabinya kidogo mnahamaki. Ooh tunaonewa!

Kila mtu afuate kilichoandikwa kwenye vitabu vya miongozo — ili siku ukiua mwanafunzi kisha wakakutia lupango usije kuanza kujinyea nyea.

Umeambiwa fukuza mtoto shule, fanya hivyo. FUKUZA.

Umeambiwa na sheria chapa bakora tatu. CHAPA BAKORA TATU. FULL STOP.

Acha kujitia ujuaji wa maadili hapa. Hauwajibiki kwa yeyote. FUATA ULICHOELEKEZWA.
 
- Matokeo ya malizi mabaya ya kumdekeza binti kumbuka kuna siku atatoka nyumbani atajichanganya kwenye sehemu ambayo haiitaji kudeka

- Matokeo ya kutokumfundisha binti kazi za ndani kumbuka kuna siku atatoka nyumbani ataolewa na kushindwa kila kitu ataachika aibu itarudi kwenu

- Matokeo ya kumtunza binti kama yai unampa vitu ambavyo ni vya hanasa kumbuka kuna siku mtafilisika atavitafuta kwa gharama nyingine sehemu nyingine au atavitumia vitu hivyo ulivyomnunulia kuharibika kwa kujiunga kwenye makundi ya ajabu

- Matokeo ya single mother kulea watoto wa kiume, kikekike, wanapopiga umbea upo naye, unapoongea na wanaume upo naye, kwenye vi part vya hovyo hovyo vya kike kike upo naye matokeo yake kumbuka kuna siku atatoka ndani atajichanganya na wanaume wenzake na hivyo vutabia alivyovirithi kwako vitakuletea aibu

- Mjini kuna tabia za hoovyo, unaweza kuwa na kabinti ndani, kakiwa ndani kanazuga kanyenyekevu kweli, kumbe ni kanyama pori

- Wazazi fuatilieni mienendo ya watoto wenu, msiwalaumu sana waalimu mnaowapelekea watoto waliopinda kwa malezi yenu mabovu, wazazi wanatengeneza general behaviour za nchi wewe mzazi unampeti peti mtoto hadi unamwaribu
 
Ndugu yangu, Haya ni maisha ya 2000 kurudi nyuma, tunaachana nayo....

Huko tuendako simu zitatumika sana mashuleni, computer ndo usiseme, magari wanafunzi wa sekondari watapaki kwenye parking za shule kutegemeana na sheria za nchi husika, kazi unazozisema zitakuwa zinafanywa na mashine.

Kama una mtoto mwenye miaka 10 kurudi chini zingatia zaidi kumfundisha HOFU YA MUNGU na skills za maisha ikiwemo exposure ya kuishi dunia yenye mazingira tofauti kabisa na yale ya kijijini tulipokulia.
 
hakuna mjualo zaidi ya mihemko tu maana hapa mmesoma uzi wa upande mmoja hamjasikiliza upande wa pili wa stori ili mpate uhalisia.

Huwezi kumhukumu mtu bila kusikiliza pande zote

Afu si ajabu mwalimu alionea gere simu ya mwanafunzi.

Yeye anamiliki techno huku mwanafunzi ana samsung galaxy.

Hapo lazima kichaa kimpande.
 
Kwahiyo "kuhisiwa" ana simu ndio inatoa tafsiri ya hayo yote uliyoandika hapo?

Ndio maana kumbe watoto wa international wako very bright kwasababu wanaishi uhalisia(usasa) kuliko hawa kayumba ambao wanaishi ujima, Imagine simu na kompyuta inaonekana ni anasa!. No wonder ndio maana mtoto anashambuliwa kama mwizi.
 
Hawa walimu ni wajinga sana.

Tena hapa walitakiwa kuwa champion wa mbele kuhimiza matumizi ya tehama shuleni.

Mradi tu pawe na utaratibu maalumu.

Maana hata hiyo elimu wanayoililia ya kuchapana mafimbo haina msaada wowote ule wala hatujaona faida zake.
 
Usimnyime mtoto mapigo kwa maana fimbo haziuwi.
Kupgwa ni haki yake sema aina ya kipigo alichopewa thathaaaa, Kiujunla ni mdekaji uyo dogo.
 
Walim wenzio unawambia nn🎤
 
Hawapo tayari kuendana na mabadiliko, wenzetu walishahama huko kwenye simu kuwa mjadala achilia mbali issue ya viboko.

Nimebahatika kupita international na kayumba kwenye level ya msingi. Akili ya mtoto wa darasa la 7 kayumba inawezekana kazidiwa na mtoto wa grade 4 international. Watoto wanakosa exposure kabisa.

Wako too inferior na ndio hawa wengi wanaohalalisha huu uharamia. Mtu kwasababu ulipigwa viboko 50 haimaanishi na mwanao apigwe viboko 60!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…