Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

Walimu 6 wa Jangwani Sekondari jijini Dar es salaam wamemhukumu kwa kumchapa makalioni fimbo 20 mwanafunzi wa kike wa kidato cha tatu na kumjeruhi vibaya kwa tuhuma za kuwa alionekana ameshika simu.

Mwalimu aliyesema hivyo alimvua nguo na kumpekua kila mahala na hakukuta simu. Alimchukua hadi ofisi ya walimu na kumlazimisha akiri lakini alikataa ndipo walimu 6 wakamshushia kipigo cha fimbo 20.

Mmoja alimchapa 5 wawili 4 kila mmoja, mmoja 3 na wawili 2 kila mmoja. Wapo walimu wa kiume na wa kike waliofanya kipigo hiki. Alipoona kipigo kina zidi aliropoka kuwa yeye hana simu bali aliye na simu ni mwenzake.

Huyo aliyetajwa kachukuliwa hatua japo mzazi alikuja kukiri binti yake kuwahi kuwa na simu.

Huyu binti aliyechapwa alihamishiwa shuleni hapo na kuishi bweni akitokea mkoani kutokana na tatizo la kiafya. Hali hiyo bado ilikuwa inamsumbua na zipo kumbukumbu katika hospitali za Dar na huko alikotoka lakini baadhi ya walimu wanasema anajifanyisha hivyo kushindikiza atolewe bweni azma ambayo wameipitisha pamoja na hicho kipigo.

Tatizo jingine ni imani kwa kuwa jitihadi za kumbadili kupitia ugonjwa zilipo shindikana wanasema haumwi.

Wapo wanafunzi walibadilishwa na kwenda upande wa hao walimu.

Tunaomba TAMISEMI, Polisi na Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto wafuatilie suala hili. Huyu binti ni mgonjwa sasa akiwa mwanafunzi wa kutwa akipata tatizo njiani nani wa kuwajibika.

Mtoto wa kike anadhalilishwa fimbo 20 shule tena kwenye makalio.

Tupaze sauti.
Hivi fimbo si zilipigwa marufuku mashuleni
 
Kuna adhabu za kuwapa watoto na sio mabakora. Ndio maana tunaonekana manyani meusi yasiyo na akili.
Mpe jembe akalime/afyeke/asafishe vyoo vya shule/apige magoti aite mvua mpaka wenzake wakitoka darasani/apewe suspension/alazimishwe asome vitabu kadhaa na aviandikie muhtasar la sivyo anafukuzwa shule n.k nk. mpe adhabu za kumjenga na sio kudhalilisha utu wake.
[emoji3][emoji3] Kuna watu mna mawazo mazuri, ila hamfikirii kama si kila wazo zuri linahitajika.
 
Nilikuwa navuta bhangi, mgomvi na siudhurii shule mara kwa mara, baada ya tukio hilo nilitubu na kuacha tabia hizo hadi sasa nina kazi nzuri na ni mtu wa mfano kwenye jamii. Wale waalimu sasa wamestaafu ni wazee kila mara nawatembelea na kuwashukuru kuwa walinirudisha kwenye ubinaadamu. Wenzangu waliacha shule, ni watu wazima ila wanaishi kitoto toto kisela na kihuni maisha ya ajabu kwa ajili ya mibange wengine wapo jela
Lakini umewahi kujiuliza mkuu swali moja: kwanini watoto wa kiafrika ndio wanaongoza kwa nidhamu mbovu kwenye maisha yao kuliko hao wasiopiga bakora watoto wao? Au napo tutasingizia ni umaskini?

Kukubadilisha wewe haiondoi dhana ya udhalilishaji uliofanyiwa mkuu. Once again pole mkuu. Tungewekeza kwenye saikoloji kama wenzetu ingetusaidia sana. Hawa watu hawapewi umuhimu ila ni muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Wenzetu ni career yenye thamani na wanapewa heshima kwa mchango wao.
 
Mkuu umemaliza huyo angepigwa hata viboko mia shenzi kabisa tunalea upumbavu sisi wenyewe na kuwapa tabu walimu....
Huna akili wewe.
Nyie ndio mnalea ujinga kwa watoto
Tupoteze muda kwa swala la malezi mabovu kwa mtoto wako. Kwanza hao walimu wangeongeza idadi zifike fimbo 100 kwa tako moja.
Ameenda kusoma au kuchati na kupiga picha walimu..
Ficha ujinga wako mkuu
 
Ulizeni mkurugenzi wa shule ya secondary scolastic kilichompata baada ya mwanafunzi wake aliekimbizwa na mwalimu wa nidhamu ili amshike bahati mbaya mtoto akadondoka na kufa kesi ilienda mahakamani na hukumu ikawatia ndani mwalimu wa nidhamu na mkurugenzi, wakati kesi inaendelea mzazi aliombwa apewe milion 100 kutoa msamaha alichowajibu je utamrudisha mwanangu akiwa hai wanakosa majibu yani ni upumbavu sana kumchapa mtoto wa mtu kwa adhabu kali je wajua mtoto ana maradhi gani je akifa bahati mbaya hivi kwanini watu hamjifunzi na matukio yanayotokea kwenye jamiii, mimi mwalimu atakae mpa mwanagu adhabu kali atalewa thamani ya mwanangu, mtoto amewashindwa mrudisheni fukuzeni mniachie mimi ni deal na mwanangu na shule zipo nyingi ni lazima asome kwenu
 
Hahaaa ww naona unalea watoto km wazungu ...hivi unawafata hao watu weusi kwa malezi huko si mtoto tu akianza hata ushoga huluusiwi kumchapa acheni kuiga kila kitu tuige vyenye tija ila adhabu kwa mtoto ni muhimu tena ya viboko
Kuna adhabu za kuwapa watoto na sio mabakora. Ndio maana tunaonekana manyani meusi yasiyo na akili.
Mpe jembe akalime/afyeke/asafishe vyoo vya shule/apige magoti aite mvua mpaka wenzake wakitoka darasani/apewe suspension/alazimishwe asome vitabu kadhaa na aviandikie muhtasar la sivyo anafukuzwa shule n.k nk. mpe adhabu za kumjenga na sio kudhalilisha utu wake.
 
usipolea mwanao vyema dunia itamfunza vyema. Mwabie simu haziruhusiwi mashuleni na adhabu yake inajulikana..ila lazima apigwe fimbo kuondoa ujinga[/I]

We jifanya kidume tu.

Siku likikupata jambo zito utabaki mwenyewe unajiliza liza.

Hata hao wanaokusapoti na kukuhamasisha kuwakatili watoto watakukimbia.

Zinabaki ama zako ama za Jamuhuri.
 
S
Simu ina shida gani endapo pakiwa na utaratibu mzuri wa matumizi yake?

Lazima sasa waalimu muanze kuwa rational, sio kupiga piga tu watoto marungu hovyo.

Siku ukimuua mtoto wa mtu, hata hizo sheria zako za shule hazitakusaidia.

Utakuwa mwenyewe ukiwa unalawitiwa na nyampara huku unajinyea hovyo.

Majuto ni mjukuu. Usije ukasema ulipitiwa na shetani, maana hata shetani atakukimbia.
Sheria, kanuni na taratibu za shule yoyote ile hapa Tz zinazuia mwanfunzi kuwa na simu kibaya zaidi simu anaitumia muda wa masomo. Mkuu acha kutetea ujinga basi.

mwalimu awe nakazi za kufundisha na kufatilia matumizi ya simu kwa mwanafunzi, tutafika kweli?


Sikubaliani na swala la mwanafunzi kutumia simu muda wa masomo..huyo mwanafunzi akiingia kwenye kumi zangu ataisoma namba.

Shule ni nidhamu bila nidhamu eti kila mwanafunzi ajiamulie aishi anavyoweza hatuwezi kufika.
 
Viboko vinasaidia na zimefelisha/kusitisha masomo wanafunzi wengi sanaa, ikiwemo..! mimi, isegekuwa viboko shulen nigekuwa na elimu kubwa sana. Ambayo nanyewe ni ubatili tu.
 
Fimb9 20 nyingi sana wamemuonea (corporal punishment) sio nzuri sana has kwa watoto wa kike.

Halafu wakike hawapaswi kuchapwa kwenye makalio wanapaswa chapwa mikononi na maximu m zisizidi 4

Usikute dogo nae nunda walimu wakaamua kumvalia kazi japo haihalalishi uzito wa adhabu walitoa.

Kuna mambo yanaweza sovika rahisi kabisa na mwanafunzi akazifeel hasara za kosa alilofanya.

Daaah ila kuna maticha hasa walw kindakindaki (old-school) wanakuaga wapuuzi sana kwenye mambo mengi.
 
Viboko vinasaidia na zimefelisha/kusitisha masomo wanafunzi wengi sanaa, ikiwemo..! mimi, isegekuwa viboko shulen nigekuwa na elimu kubwa sana. Ambayo nanyewe ni ubatili tu.
Mbona seminary hakuna viboko na watoto wana nidhamu ya hali ya juu, hawa walimu wa kidigitali ni wapuzi sana wanahisi mtoto hafundisiki bila viboko wewe umesikia wapi, shule bora ni zile zinazofundisha nidhamu kww approach mbalimbali, mwanngu yupo shule ambayo hawatumii viboko bali wana njia za kumkuza mtoto maadili, na mwanangu tangu aanze pale amekua anafaulu na adabu nidhamu za hali ya juu,
 
We jifanya kidume tu.

Siku likikupata jambo zito utabaki mwenyewe unajiliza liza.

Hata hao wanaokusapoti na kukuhamasisha kuwakatili watoto watakukimbia.

Zinabaki ama zako ama za Jamuhuri.
Ukitaka hivyo kila mtu afate sheria.
Mbona huyo mwanafunzi hajafata sheria zinazo zuia kutumia na kumiliki simu shuleni.

Mbona hawa watoto mnawatetea sana kiasi kwamba wao ni spesheli sana. Shule ni nidhamu bila nidhamu hilo ni kundi la vibaka.

Hata huko kanisani kuna taratibu zake iweje chombo kinachozalisha wasomi na wataalam ndiyo waishi kienyeji..lazima wafunzwe adabu akiwa jeuri ni kimpasua kichwa..
 
We jifanya kidume tu.

Siku likikupata jambo zito utabaki mwenyewe unajiliza liza.

Hata hao wanaokusapoti na kukuhamasisha kuwakatili watoto watakukimbia.

Zinabaki ama zako ama za Jamuhuri.
Ukitaka hivyo kila mtu afate sheria.
Mbona huyo mwanafunzi hajafata sheria zinazo zuia kutumia na kumiliki simu shuleni.

Mbona hawa watoto mnawatetea sana kiasi kwamba wao ni spesheli sana. Shule ni nidhamu bila nidhamu hilo ni kundi la vibaka.

Hata huko kanisani kuna taratibu zake iweje chombo kinachozalisha wasomi na wataalam ndiyo waishi kienyeji..lazima wafunzwe adabu akiwa jeuri ni kimpasua kichwa..
 
Fimbo haziepukiki usipowachapa unazalisha taifa lisilo na nidhamu wala kufuata maadili.

Kama hutaki mwanao achapwe mchukuw mfundishe nyumbani kwako.

Sisi wengi tumekula sana mbata shule imetushape hivi tulivyo lasivyo tungekuwa vijana wa ovyo
 
Back
Top Bottom