Mwanafunzi Chuo cha Ufundi Arusha amuua mwenzake akimdai Tsh. 3000

Mwanafunzi Chuo cha Ufundi Arusha amuua mwenzake akimdai Tsh. 3000

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
753
Reaction score
1,812
Mwanafunzi Ibrahim Shaaban wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) anashikiliwa na polisi Mkoani Arusha Kwa kosa la kumuua mwenzake Evance Florian (17) katika ugomvi wa kudaiana sh, 3000.

Kamanda wa polisi Mkoa hapa Justine Masejo amethibitisha tukio hilo na kudai kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospital ya rufaa Mount Meru huku mtuhumiwa akishikiliwa na polisi Kwa uchunguzi zaidi.
 
Mwisho wa mwaka hua kuna kila aina ya maovu
 
Mwanafunzi Ibrahim Shaaban wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) anashikiliwa na polisi Mkoani Arusha Kwa kosa la kumuua mwenzake Evance Florian (17) katika ugomvi wa kudaiana sh, 3000.

Kamanda wa polisi Mkoa hapa Justine Masejo amethibitisha tukio hilo na kudai kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospital ya rufaa Mount Meru huku mtuhumiwa akishikiliwa na polisi Kwa uchunguzi zaidi.
Nchi ya uchumi wa kati......
Hii ni indication ya kukua kwa umaskini
 
Majaribu ni mtaji wa imani.

Wanadai kipimo cha imani ya wakomunisti ilikuwa ni pale ilipokuja njaa, kila mmoja alikimbilia mkate na ile spirit of communism sharing. Tanzania tumesifiana kwa miongo kadhaa kuwa sisi ni watu wa amani na tukasahau kuwa amani hiyo ilijengwa na misingi ya haki.
Kwa hali ilivyo mtaani kiuhalisia hata binafsi nimeanza kuamini kuwa mbele ya pesa sisi sio watu na mbaya zaidi hatujafundishwa kiuhalisia misimgi ya upendo na kuvumiiana bali tunaigiza tu.

Kuna mambo ya ajabu sana na huenda tukashuhudia madhara zaidi.
 
Back
Top Bottom