Mwanafunzi Chuo kikuu cha Dodoma ajirusha kutoka Ghorofani.. anusurika kufa!!

Mwanafunzi Chuo kikuu cha Dodoma ajirusha kutoka Ghorofani.. anusurika kufa!!

Down To Earth

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
21,940
Reaction score
16,643
1.png


Mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu Dodoma – UDOM aliyefahamika kwa jina la KAMUGISHA S/O ISACK, Miaka 24, Mwaka wa Tatu, Kitivo cha Sayansi ya Jamii (Social Science) anayeishi Block Namba 11, chumba Namba 62, alijitupa kutoka ghorofa ya pili hadi chini na kusababisha majeraha sehemu za mdomoni, shingoni na paji la uso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amesema tukio hili limetokea terehe 18/03/2014 majira ya 20:15 huko maeneo ya chuo kikuu cha Dodoma manispaa na Mkoa wa Dodoma.

Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi. Majeruhi alilazwa katika hospitali ya UDOM na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na kuruhusiwa tarehe 20/03/2014 baada ya kuonekana hali yake inaendelea kuimarika.

Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilisha taratibu zote kujibu shitaka la kujaribu kujiua.

 
Kumbe Hata WAHAYA wapumbavu wapo eh! Ama hakika kwenye Mbio za mamba kenge hawakosekani.
 
Mkuu kwani ni lazima umtaje kabila?, lakin pia siamin kama kweli wanafunzi wa chuo kitukufu cha UDOM wanaweza kufanya ujuha huo huenda ni mwanafunzi wa CBE, St.Johnes au chuo cha mipango maana wanafunzi wake huwa hawajitambui.

IDUMU UDOM MILELE.
 
Mi nna wasi wasi wenda jamaa kapigwa red card na dem wake!!! Alafu wanasema pombe!!
 
Mkuu lazima umatej kabila, lakin pia siamin kama kweli wanafunzi wa chuo kitukufu cha UDOM wanaweza kufanya ujuha huo huenda ni mwanafunzi wa CBE, St.Johnes au chuo cha mipango maana wanafunzi wake huwa hawajimtabui.

IDUMU UDOM MILELE.

we jamaa wa wap inaonekana upo mwaka wa kwanza hapo udom na hujaelewa maana ya elimu mbumbumbu mkubwa
 
Back
Top Bottom