JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari Mpakani Ufunuo Mwamlima (13) mkazi wa mtaa wa Chapwa A Halmshauri ya mji wa Tunduma mkoani Songwe amejichoma kisu cha tumboni hadi kufa baada ya wazazi wake kumhoji juu ya mwenendo wa tabia zake ambazo zimeonesha kutokuwaridhisha wazazi.
Kijana huyo amechukua maamuzi hayo baada ya wazazi kumhoji kwa tuhuma walizozipokea toka kwa majirani ambapo walimtuhumu kwa wizi wa fedha katika kibanda cha Nyumbani kwao pamoja na kutohudhuria masomo shuleni.
Akizungumza kwa niaba ya Familia baba mkubwa wa Marehemu Fadhiri Mwamlima amesema kuwa usiku wa Septemba 10,2024 baada ya wazazi wake kumuita kijana wao kumhoji juu ya matukio ya wizi wa hela kwenye kibanda chao ndipo kijana alikiri kuwa na chenji alizodai anaenda kuzichukua ili awaletee na baadaye walisikia kelele kutoka jikoni.
Mwamlima amesema mtoto huyo alikiri kuiba fedha zinazotokana na mauzo ya duka lililopo nyumbani ,baada ya kubaini kuporomoka kwa duka hilo ambapo alihpoulizwa kijana huyo kwa mara ya kwana alikana na baadye kukubali kama anaiba fedha kwenda kulia shuleni.
“Baada ya kukiri akuiba fedha hizo alisema chenji zipo chumbani alipokuwa kama anaingia chumbani aliingia jikoni kuchukua kisu na kumuaga mdogo wake kwa kumpungia mkono, na baadaye akajichoma na kisu tumboni,” amesema Mwamlima.
Amesema walipotoka walikuta kijana amejichoma kisu na utumbo uko nje na walipojaribu kumkimbiza hospitali kijana alifariki akiwa njiani.
Mwenyekiti wa mtaa wa Chapwa A Steven Minga amesema alipokea taarifa kutoka kwa balozi wake na namna ulivyotokea licha ya jitihada za kuokoa uhai wa mtoto huyo lakini umauti ulimkuta baada ya kufika hospitali.
Diwani wa kata ya Chapwa Jackson Siame ametoa rai kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao ikiwepo kuzuia kuangalia filamu zenye maudhui ya kujiua ili kujiepusha na matukio ya mauaji kama yaliyomkuta kijana huyu.
"Tujaribu kuwaepusha vijana wetu kuangalia filamu hizi wanazoangalia ukiangalia kijana huyu amefanya tukio hili kwa ujasiri huenda imetokana na ujasiri wanaoungalia pindi wanapoangalia maudhui ya filamu hizo," amesema Siame.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe Gallus Hyera amethibitisa kutokea kwa tukio hilo huku akishauri jamii ionapo mwananchi ana msongo wa mawazo wajuwe namna ya kulitatua ili kuepusha vifo vya watu kujiua.
Chanzo: Habarijamiitanzania