Mwanafunzi MUCCOBS Apoteza maisha kwa kipigo

Apex

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
425
Reaction score
61
Ni mwanafunzi wa mwaka wa pili suleiman John BAMFED juzi jumatatu alivamiwa na watu wasiojulikana majira ya usiku maeneo ya shule ya secondary old moshi na kupigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa na ncha kali..mwanafunzi huyo alipelekwa hospitali lakini juhudi za madaktari za kuyaokoa maisha yake hazikusaidia. Jana majira ya asubuhi alipoteza maisha !!!

Marehemu ataagwa leo mchana ukumbi wa Mwl Julias K nyerere(JK HALL) tayari kwa kusafirishwa kuelekea shinyanga. RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE,APUMZIKE KWA AMANI....AMINA
 
Jamani mbona haya mambo yanatisha sasa.
R.I.P. kijana.
 
Naomba ututajie sababu ni nini?ila nahis sababu huweza kuwa siasa,mapenzi,pombe.
 
Naomba ututajie sababu ni nini?ila nahis sababu huweza kuwa siasa,mapenzi,pombe.

mpaka sasa sababu hazijawekwa wazi na mbaya zaidi marehemu hakuweza hata kusema neno lolote kabla ya mauti hayo. Anyway nitaendelea kuja hapa kwa taarifa zaidi kama nikizipata..
 


Nigeshangaa sana mwaka kupita bila SUA wala branch yake kumpotezaa mtu.?! sijui kuna shida gani maana kwa miaka mitatu mfululizo hilo jambo linajirudia. Ok ni mipango ya Mungu, RIP Best. God bless SUA.
 

Kwani we ni POLISI mkuu???
 
yaani watanganyika kila siku ni kuuana,kuchinjana etc.

Huko geita tena wamechinja mwanamke mmoja,duh!!

Ukimuuliza yule Njegele... atakwambia ni maendeleo, si hata foleni alisema hivyo hivyo..!?
 
Kuna vifo vingi sasa vya namna hii vinavyowakumba wanafunzi wa vyuo vikuu tanzania pamoja na kuibiwa, kujeruhiwa na hata kubakwa.
Ifikie mahali sasa serikali iweke sheria na utaratibu kwa vyuo vyote nchini kuwapa malazi ya nyumba(hostels) wanafunzi ili wakae kwa pamoja ambapo inakua rahisi kuwalinda kuliko hii ya kila mmoja ajitafutie malazi.
 
RIP kijana
mpigamsuli njoo hapa kijana tujue umzima
 
Last edited by a moderator:
R.i.p Bro umetangulia sisi bado atujajua ni lini tutafika mwisho na tutakufa kifo gani.RIP. BRO.
 
R.I.P brother,poleni jirani zetu wa muccobs Mungu awatie nguvu.Marehemu alilazwa icu hapa KCMC ila hakuweza kuzungumza chochote.
 
Poleni sana ndg.the nation isnt aware of its future pillars.every one dipping in Polishit and forget what the future needs for its development,ila muccobs tulieni mnatuchosha kwa mambo mabaya Moshi. Muogopeni Mungu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…