Mwanafunzi UDOM aibuka mshindi kwa kubuni Nembo ya Made in Tanzania

Tuachane na nembo em tujue familia, ndugu na jamaa za mshindi ili tusiwaze kama ni baba kantuma.
 
Dah kmmk hy nendo Ndo Namba moja? Ah bc ya mwisho itakuwa kituko cha dunia 🙌
Ila Tz kwenye ubunifu ni 0 guys
 
Wakunyumba ametuwakilisha vyemaa!!
Bombiii Nyumbiii hoyeeee!!
 
Tanzania kweli tupo nyuma ya technology.

Kitu AI inafanya kwa sekunde eti mpaka uitishe shindano, nonsense.
Mkuu hata waliotengeneza hizi tech bado wanatumia binadamu. Mfano canva bado wanatumia binadamu kuhakiki template zao na kwa kiswahili wanamlipa $14 kwa saa ya uhakiki.
 
Hongera kwake
 
Mimi nimeshika nafasi ya pili Mkuu. Namshukuru Mola Muumba kwa hilo. Asanteni sana wana jamii forum kwa support yenu
Tuonyeshe ya kwako inaweza nzuri zaidi ya hii
labda wamekuchakachua, si unajua tena hii nchi....
 
Sasa hata huyo si wazi katumia AI, tofauti ipo wapi?

Hivi hata ukifananisha huyu wa sasa na yule akiyegundua nembo ya bibi na bwana, yupi haswa ni kichwa kuzidi mwenzake?
Logo au nembo nowadays hazihitaji mambo mengi,

Angalia mfano Logo ya Juventus ,Luis Vuitton,n.k

Huyo mshindi ni sahihi kabisa

Kwasasa ,logo duniani ni zile zenye vitu vichache zaidi, angalia hata logo ya klabu ya Simba ya zamani na sasa ,

Unaiona ile logo ya Yanga ,ile ni ya kizaman sana ,wakipewa tenda wazabuni na wabunifu, utashangaa itakayishinda ,
 
Tuonyeshe ya kwako inaweza nzuri zaidi ya hii
labda wamekuchakachua, si unajua tena hii nchi....
Hapana hawajachakachua Boss. Kura zilizopigwa zilikuwa ziko wazi na kijana wa UDOM aliongoza kwa asilimia 50 dhidi ya asilimia zangu 42. Hapa chini nitakuthobitishia hilo na pia ninakuwekea nembo zilizoifikia hatua ya 3 bora. Ya kwangu ni hiyo A.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…