PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Serikali imetakiwa kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa Waraka wa Elimu Na. 24 wa mwaka 2002 unaoweka mwongozo wa utoaji wa adhabu ya viboko shuleni, baada ya kubainika kuwa baadhi ya shule zimekuwa zikikiuka masharti yaliyowekwa.
Jukwaa la Watoto Tanzania limedai kuwa ukiukwaji huo unaweza kuathiri kujiamini kwa wanafunzi na kuwafanya baadhi yao kushindwa kutimiza ndoto zao kutokana na athari za adhabu wanazopata shuleni.
Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Daniel Magembe amesema hayo jijini Dodoma wakati wa Jukwaa la Baraza la Watoto Kitaifa, akisisitiza umuhimu wa Serikali kuhakikisha miongozo inayosimamia utoaji wa adhabu shuleni inatekelezwa ipasavyo.