Mwanafunzi wa chuo ajishindia Tsh bilioni 4 kwa kubeti kwa usahihi mechi 17

Mwanafunzi wa chuo ajishindia Tsh bilioni 4 kwa kubeti kwa usahihi mechi 17

crankshaft

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,427
Reaction score
3,438
Mwanafunzi Eli Kipruto 22 wa Jomo Kenyatta University Kenya kajishindia ksh 200M(karibu bilioni 4 za kitanzania) baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 17 kwenye kampuni ya betika.

Pamoja na ushindi huo akihojiwa kijana huyo amesema anataka amalize shule na hana mpango wa kuoa.

Chanzo: NTV Kenya
===
53695e4c8e520664.jpg


Eli Kipruto (22) mwanafunzi wa IT, Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT) amekuwa mshindi wa kitita hicho baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 17 na alitumia KES 49 ambayo ni sawa na TZS 927.

Kijana huyo amekuwa akibashiri kwa miaka mingi bila mafanikio lakini sasa ameingia kwenye orodha ya mamilionea wa Kenya. Amepanga kuwajengea nyumba wazazi wake na kuendelea na elimu ya chuo, huku akisema hana mpango wa kuoa.
 
Mwanafunzi eli kipruto 22 wa jomo kenyata university kenya kajishindia ksh 200M(karibu bilioni 4 za kitanzania) baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 17 kwenye kampuni ya betika.

pamoja na ushindi huo akihojiwa kijana huyo amesema anataka amalize shule na hana mpango wa kuoa
source: ntv kenya
Nikajua mwanafunzi wa Muslim University of Morogoro kashinda bet
 
Watu na upepo wao,
Ingia kichwa kichwa sasa na nuksi + mikosi ya babu zako huko walizulumiana mipaka ya mashamba.
Hushindi kitu, halafu unaambiwa unadaiwa na Betika umeiibia, au unaweka pesa huioni..
Hata ukishinda hupewi, ukienda kudai unashtakiwa unaleta utapeli kwenye kampuni ya watu.
 
Badala aseme atazifanyia nini hizo hela ye anatanguliza hataki kuoa. Duuh.

Sema bana si ajabu akazitumia kuendelea kubet mpaka mwisho wa siku zinarudi zilipotoka.
 
Fala sana, shule ya nini anaendelea nayo?
Mkuu acha asome tu huenda akawa na uwanja mpana wa namna ya kutumia hiyo hela.

Hujagongana na ule uzi wa yule jamaa pale Kkoo anayedai kwa anadaiwa b.4 na benki ambazo alizikopa na kuzifanyia biashara , mwisho wa siku kazipeleka kwenye madini zikapukutika zote na mpaka sasa hana hata sumni na namna ya kurudisha deni pia hana amebakia ana haha.
 
Back
Top Bottom