Mwanafunzi wa darasa la saba afariki kwa shoti ya umeme akichezea Brenda ya Juice

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi St. Louis wilaya ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro, aitwae Ian Macha (13), amefariki dunia, ikidaiwa kuwa ni baada kupigwa shoti wakati akijaribu kuingiza waya wa blenda kwenye swichi ya umeme, kwa lengo la kufanya mchezo usiku wa August 3, 2026, wilayani humo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizonakiliwa na GADI TV kutoka kwa Irine Temu ambaye ni mama mdogo wa marehemu huyo, zinasema kuwa "alikuwa anaweka waya wa mota ya brenda kwenye soketi ya umeme chumbani kwake, akapigwa shoti, hakukuwa na jagi, na alifia mapokezi hospitalini" amesema Irine.

Aidha, Irine amesema kuwa ibada ya mazishi ya mwili wa mtoto huyo yanatarajiwa kufanyika August 8, 2026 huko katika maeneo ya Soweto wilayani humo.

1786167949716.png
 
Kama mzazi nimejifunza kitu kupitia hili tukio. Poleni wafiwa kwa msiba wa kijana wenu mdogo.
Duh mimi nilijua umeme wa ndani unashtua tu. Zamani utotoni kulikuwa na switch ya taa waya ziko nje. Tulikuwa tunaenda kugusa na kutetemeshwa ikawa ndio mchezo wetu!
 
Umeme unapiga vibaya nikiwa mdogo niliingiza chuma kwenye soketi nilihisi kuna nguvu imenipiga kuanzia juu hadi chini bahati nzuri niliachia ile chuma
 
Duh mimi nilijua umeme wa ndani unashtua tu. Zamani utotoni kulikuwa na switch ya taa waya ziko nje. Tulikuwa tunaenda kugusa na kutetemeshwa ikawa ndio mchezo wetu!
Generally domestic Power sio kubwa ya kuleta maafa, ni Low Voltage energy.

Possibly alishika kwa mikono miwili na akawa kwenye bare surface yenye conductor kama maji hivi.

It is very sad, hata hivyo kifo ni kifo tu
 
Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi St. Louis wilaya ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro, aitwae Ian Macha (13), amefariki dunia, ikidaiwa kuwa ni baada kupigwa shoti wakati akijaribu kuingiza waya wa blenda kwenye swichi ya umeme, kwa lengo la kufanya mchezo usiku wa August 3, 2026, wilayani humo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizonakiliwa na GADI TV kutoka kwa Irine Temu ambaye ni mama mdogo wa marehemu huyo, zinasema kuwa "alikuwa anaweka waya wa mota ya brenda kwenye soketi ya umeme chumbani kwake, akapigwa shoti, hakukuwa na jagi, na alifia mapokezi hospitalini" amesema Irine.

Aidha, Irine amesema kuwa ibada ya mazishi ya mwili wa mtoto huyo yanatarajiwa kufanyika August 8, 2026 huko katika maeneo ya Soweto wilayani humo.

Niwape pole wazazi wake this is so so hard to them, watu wasikie tu.

Mostly rip to young man
 
Pole sana watoto wetu wengi ni watundu sana tujaribu kuwasihi apumzike kwa Amani 😢 🙏
 
Poleni sana wafiwa, ila kuna uzembe mkubwa sana wa wazazi kwenye hii situation.
 
Mimi nilijua umeme wa majumbani hauui sasa watoto si wako hatarini?
 
Back
Top Bottom