Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wewe ni mwanafuni unayejiandaa kwenda kidato cha 5 ukiwa na ndoto ya kusoma tahasusi fulani, lakini unajikuta umepangiwa tahasusi tofauti na matarajio yako, na wakati mwingine unapangiwa tahasusi uliyochagua lakini kutokana na sababu mbalimbali unafikia maamuzi ya kubadili tahasusi hiyo, je, unatakiwa kufanya nini?
Jamii Forums imefanya mazungumzo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah na kupata ufafanuzi juu ya suala hili, ambapo ameeleza:
Kwanza kabla ya kufikiria kuhama tahasusi husika mwanafunzi anatakiwa kuzingatia kama ana alama za kutosha (cut-off points) zinazomuwezesha kusoma tahasusi husika, kama shule husika ina tahasushi hiyo, lakini pia kama kuna nafasi zaidi ya yeye kuweza kuongezeka sababu wakati mwingine shule inaweza kuwa na tahasusi hiyo lakini nafasi zimejaa kulingana na miundombinu ya shule hiyo.
Kama kila kitu kipo sawa mwanafunzi atatakiwa kuandika barua kwa Katibu Mkuu wa TAMISEMI aeleze anachokutana nacho, na ambacho hajaridhika nacho na kile anachoamini anastahili kukipata. Wakiipokea wataichambua wakiona kama ana sifa basi watambadilishia.
Je, mwanafunzi anaruhusiwa kuhama Tahasusi baada ya muda gani?
Hosseah anafafanua, muda sahihi kwa mwanafunzi kuhama Tahasusi ni wiki mbili au tatu za mwanzo baada ya shule kufunguliwa.
Ikiwa mwanafunzi amekumbana na changamoto au hajaridhirika na maamuzi yaliyotolewa, anapaswa kupeleka malamaiko kwa Katibu Mkuu TAMISEMI kwa kuandika barua na kuelezea anachokutana nacho, na maamuzi zaidi yatafikiwa.
PIA SOMA
- TAMISEMI wafafanua kinachopelekea wanafunzi Kupangiwa Tahasusi (Combinations) tofauti na machaguo yao