Mwanafunzi wa miaka 14 ahukumiwa kuchapwa Viboko kwa kumbaka Mtoto wa miaka 7 Gairo

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mahakama ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro Aprili 4, 2025 imemhukumu adhabu ya viboko 5 gerezani Chrispin Matei Malanda (14) mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari Gairo, kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 7 anayesoma darasa la pili kwenye moja ya shule ya msingi iliyopo wilayani hapo.

Mama wa mtoto huyo (jina limehifadhiwa) mkazi wa mtaa wa Kisimani wilaya ya Gairo aligundua kubakwa kwa mtoto wake baada ya kuona akitembea kwa maumivu na kuchukua hatua za kumpeleke katika kituo cha Polisi Gairo na kuanza upelelezi.

Jeshi la Polisi wilaya ya Gairo lilimbaini na kumkamata Chrispin Matei Malanda kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo alilolitekeleza baada ya kumvizia mtoto huyo akiwa anacheza na watoto wenzake kisha kumpeleka vichakani na kumbaka.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amesemna chanzo cha tukio hilo ni mmomonyoko wa maadili pamoja na kukosekana kwa usimamizi wa watoto wanapokuwa michezoni.
 
kwa bahati mbaya hiyo ndio sheria ilivyo kwa tz, nadhani kuna umuhimu umri wa watoto wanaogombana na sheria upunguzwe, waende gerezani kwa sababu kwa mzazi wa mtoto aliyebakwa kuja kuona mtoto kama huyo yupo nje kwa viboko tu, kwa uelewa wa watanzania, usalama wa huyo mbakaji ni mdogo sana huku nje, bora akae ndani kwa usalama wake. usifanye mchezo na mtoto wewe, ati unasikia kijana fulani kambaka.
 
Back
Top Bottom