Kama sio ujinga basi ni utoto. Kama kila anayepigwa chini angekuwa anajinyonga basi tungekwisha maana watu wengi wamepitia hatua hiyo. Tatizo vijana wengi siku hizi hawasomi kuelewa bali wanasoma kukariri tuu ili mradi afauli. Kuna misemo mingi tunaisoma kila siku. kwa mfano, asiyekubali kushindwa si mshindani, usiangalie ulipoangukia, angalia ulipojikwaa ili usijikwae tena.
Mimi nimesoma hapo UDSM miaka minne, nilikuwa na mwanamke mwaka wa kwanza akanizingua na kunipiga chini, kuanzia pale sikuwa na demu mpaka nilipomaliza chuo. Leo nina kazi nzuri sana na maisha mazuri na familia yangu. tena wasichana ndo wananishobokea sana, japo sina time nao.
Vijana wanatakiwa waelewe kuwa wasikimbilie mapenzi bila kukomaa kisaikolojia, ni hayo tuu kwa leo.