Mwanafunzi wa mwaka wa pili udsm,akutwa amejinyonga.

Mwanafunzi wa mwaka wa pili udsm,akutwa amejinyonga.

Perry

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
10,058
Reaction score
2,195
Ni mwanafunzi wa mwaka wa pili anaechukua sheria,ameacha kikaratasi kinachosema amejiua sababu ya ugumu wa maisha.lakini kwa mujibu wa watu wake wa karibu wanasema,msela amepigwa chini na girlfriend wake ndo akaamua kuchukua uamuzi huo..mungu ailaze roho yake mahali panapo stahili.
 
Tatizo vijana wengi siku hizi hawajiandai kisaikolojia, akishapigwa chini na 'boyfriend/girlfriend' anaona bora kujiua.
Mbona kuna watu walipigwa chini na wakajipa moyo na maisha yakaendelea?
Huu msongo wa maisha na kutokubali matokeo kutakwisha lini kwa vijana wetu?
MUNGU AMREHEMU!
 
hatua mbaya sana kuwahi kufikiwa kwenye historia ya mapenzi...
 
Kama sio ujinga basi ni utoto. Kama kila anayepigwa chini angekuwa anajinyonga basi tungekwisha maana watu wengi wamepitia hatua hiyo. Tatizo vijana wengi siku hizi hawasomi kuelewa bali wanasoma kukariri tuu ili mradi afauli. Kuna misemo mingi tunaisoma kila siku. kwa mfano, asiyekubali kushindwa si mshindani, usiangalie ulipoangukia, angalia ulipojikwaa ili usijikwae tena.

Mimi nimesoma hapo UDSM miaka minne, nilikuwa na mwanamke mwaka wa kwanza akanizingua na kunipiga chini, kuanzia pale sikuwa na demu mpaka nilipomaliza chuo. Leo nina kazi nzuri sana na maisha mazuri na familia yangu. tena wasichana ndo wananishobokea sana, japo sina time nao.

Vijana wanatakiwa waelewe kuwa wasikimbilie mapenzi bila kukomaa kisaikolojia, ni hayo tuu kwa leo.
 
kweli kabisa mimi mwenyewe nimesoma enginering telecom kama kupigwa chini ndo kujiua basi ningejiua zaidi ya mara 3 mana nishapigwa chini na mtu niliemgarmia sana kumbe alikua na mtu lakini maisha yalisonga ...na sasa watu tuna kazi nzuri balaa lipo kwao maana naweza nikakupiga chini mda wowote coz nilishajifunza na wala sitaki longolongo na mademu...elimu yenyewe tumeipata kwa tabu kila cku kunji ..kazi zenyewe tumezisotea sana ....labda jamani tuulize huyu mtu alikua kabila gani? maana makabila mengne huitaji kuuliza ukckia amejiua
 
Mmh, Mwenyezi Mungu awalinde watoto wetu huko waliko.
 
Naanza kuongea na wanangu kuhusu mahusiano mapemaaa

Wajue siku moja wataumizwa sana mioyo, sio mwisho wa maisha, kila mmoja anapitia kwa wakati wake
Wajue sio kitu cha ajabu, ndio maisha yalivyo
 
Wanayaingia mapenzi bila kujua gharama yake kamili. RIP.
 
Mimi pia nimethibitisha kwa macho yangu baada ya kupata taarifa hiyo toka kwa mwanafunzi aliyekuwa anaenda darasani pia kwa RPC Kenyela.
Kiufupi ni kwamba Huyo mwanafunzi alikua anasoma mwaka wa pili sheria siyo wa tatu, pia kwenye karatasi niliyoina mwenyewe hamna anaposema ugumu wa maisha. Mojawapo ya maandiko yake ni "Nimekufa mwenyewe na Mungu pekee anajua kifo cha mja wake, ndugu zangu ishini kwa upendo amani" pia ameelekeza pa kuzikwa.

Nafikiri cha kujadili siyo kile kilichomfanya yeye afe maana hatukijui ila ni nini kinachopelekea mtu ajiue na namna gani tusaidiane kuepuka hilo? Maana kihistiria huyu bwana alishatangaza kujiondoa marafiki zake wakaona ni malaria wakampeleka hosipitali wakaambiwa ni msongo wa mawazo. Swala la ugumu wa maisha silioni hapo maana amekutwa kiasi fulani cha fedha mfukukoni amelipa ada na aalikua analala mabibo hostel. Mwandishi wa Dailynews amenikuta pale kituo cha polisi chuo kikuu, yeye kapewa nafasi ya kuongea na rafiki zake wa karibu sana ambaoamewataja kwenye andiko aliloacha kuwa walimsaidia kuokoa maisha yake lakini ikashindikana. labda kesho tutasoma vyema kuhusu hilo kwenye dailynews.

Swala la kuwa ni girlfriend sijui kitu gani tuachane nayo maana hakuna mwenye uhakika na hilo. Waswahili tunasema msiba usikie kwa wengine ukija kwako utaipata. Yakikukuta ndugu haya tunayoandika kwa kukebehi humu jf unayasahau yote unaona kona zote mbinu zote hazifai linalofaa ni kuondoka nje ya uso wa dunia.
 
Dah inasikitisha sana mana sio mara ya kwanza mwanafunzi kujinyonga mi naona imefika wakati sasa serikali iandae tume ya kuchunguza haya majanga RIP
 
Inaa rilah wa inarirah rajuun...polen xana wana udsm na taifa kwa ujuml koz 2mepoteza ngv kaz
 
Kaacha noti akisema ugumu wa maisha, nyie mnawatafuta masela ili waseme nini ilhali yeye kawaambia ugumu wa maisha?
 
vijana wengi wana ulimbukeni wa mapenzi, binafsi masomo kwanza, hawa mabinti wapo tu, tena unapopata kazi unabadili kama nguo ila UKIMWI upo, RIP
 
Back
Top Bottom