Mwanafunzi wa sekondari apatikana akiwa na bunduki shuleni Kenya

Mwanafunzi wa sekondari apatikana akiwa na bunduki shuleni Kenya

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari katika kaunti ya Homabay nchini Kenya, anashikiliwa na polisi akitarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kupatikana akiwa na bunduki, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation.

Mwanafunzi huyo wa umri wa miaka 17 alikamatwa siku ya Jumanne baada ya wanafunzi wawili kuripoti kuwa amekuwa akiwatisha kwa bunduki hiyo.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Dickens Bula, alisema kuwa usimamizi wa shule ulijulishwa na wanafunzi waliodai kuwa mwenzao amekuwa akiwatisha kuwa angewapiga risasi.

Gezeti hilo linasema kuwa baada ya mwanafunzi huyo kukamatwa na kuhojiwa, aliwapeleka polisi kwa kichaka kilichokuwa karibu ambapo alikuwa ameificha bunduki hiyo.

Daily Nation linasema kuwa bunduki hiyo ni ya kimarekani na hajaruhusiwa kutumiwa nchini Kenya.

Linasema kuwa licha ya uchunguzi kugundua kuwa bunduki hiyo haikuwa na risasi, usimamizi wa shule na wanafunzi walishikwa na hofu, na kusababsisha wanafunzi zaidi kuhojiwa kuhusu silaha hiyo.

Mkuu wa polisi eneo hilo Esau Ochorokodi, alisema mwanafunzi huyo aliwaambia wachunguzi kuwa alipata bunduki hiyo kutoka kwa jamaa wake anayeishi nchini Marekani.

Sasa mwanafunzi huyo anasubiri kushtakiwa kwa kumiliki bunduki bila kibali katika hakama ya Homa Bay.

BBC Swahili
 
Ningekuwa na bunduki nikiwa shule ya sekondari singekosa wa kupiga risasi! Yaani akili zangu za kitoto zilifanya niwachukie sana watu niliowaona ni kama wanaongeza ugumu wa hali yangu ya maisha shuleni. Sasa hivi hao hao watu nikiwakumbuka huwa kimoyomoyo naambia Mungu awabariki sana.
 
Back
Top Bottom