Mwanafunzi wa sekondari apunguziwe mzigo wa masomo kwa mtindo huu

Mwanafunzi wa sekondari apunguziwe mzigo wa masomo kwa mtindo huu

Umeweka masomo ambayo hayatusaidii chochote Maishani ni sawa.

Ila pia ningependa kabla hatujaendelea uweke list ya masomo yanayotusaidia na uweke hizo faida pia japo kwa uchache tu.
Mkuu acha utani, kama umesoma digrii/diploma ya kiswahili isiwe sababu ya kutetea yasiotufaa.
Masomo yanayofaa ktk mazingira ni biashara,kilimo,jografia,science,hisabati na ict. Mengine ni utopolo.
 
Madhumuni ya elimu ni kuongeza ufahamu na maarifa ya kukabili mazingira yako. Hebu niambie huoni umuhimu wa kujua historia? Civics haikuongezei maarifa kweli?

Vv
Maarifa unapata lakini kwa ulimwengu wa leo umuhimu wake ni mdogo. Dunia inamaarifa kibao, huwezi kuwa nayo yote. Lazima tuangalie yale yaliyonafaa zaidi na kukomaa nayo bila kukengeushwa na yale yasiyo na manufaa au yenye manufaa kidogo.
 
Cha ajabu kuna watu wengi hawajafika hata sekondari lakini wanaishi na wanapambana na mazingira sasa iweje ulazimishe wanaofika sec wasome kila kitu wakati hakuna wanachowazidi wale walioshia la saba.Hivi mtu wa sekondari ambaye hajaenda chuo chochote anamzidi nini wa std7.
 
Mkuu acha utani, kama umesoma digrii/diploma ya kiswahili isiwe sababu ya kutetea yasiotufaa.
Masomo yanayofaa ktk mazingira ni biashara,kilimo,jografia,science,hisabati na ict. Mengine ni utopolo.

Sawa mkuu ila sidhani kama mchango wangu ulikuwa kutetea !! Nadhani ombi lakini pia kwenye maada yoyote si busara wote kuwa na mawazo sawa mnapoanza kujadili!! Ila mwisho wa mada.
 
Biolojia inatusaidia kujua mwili na afya zetu, fizikia ndiyo msingi wa ufundi, hesabu tunatumia kila siku. Chemistry, tunatumia kila siku kemikali jiografi na kiingereza ni muhimu sana.
Kama umeona Kiingereza ni muhimu, basi na Kiswahili vile vile. Hata uzi wako umewasilisha katika Kiswahili, vipi hutaki kieleweke kwa undani?

Uraia nafikiri ndio civics. Liwepo na liboreshwe kwa kujikita zaidi katika mambo ya katiba ya nchi na sheria. Hii iwaondolee WaTz woga na umbumbumbu wa haki/ wajibu zao za msingi ambazo kadiri siku zinavyokwenda, wanasiasa uchwara na majeshi ya nchi yanazidi kuzisigina.

Historia inaweza ikafundishwa kwa kusimuliana kama ulivyopendekeza.
 
Cha ajabu kuna watu wengi hawajafika hata sekondari lakini wanaishi na wanapambana na mazingira sasa iweje ulazimishe wanaofika sec wasome kila kitu wakati hakuna wanachowazidi wale walioshia la saba.Hivi mtu wa sekondari ambaye hajaenda chuo chochote anamzidi nini wa std7.
Mtu wa form 4 na la saba hamna walichozidiana labda, kiingereza. Na kuna la saba wengine wanapiga ngeli kuliko hao form 4. Kuna jamaa yangu tulipomaliza form 4 credits hazikutosha, akaenda kuwa saidia fundi kwa fundi wa la saba. Tunatakiwa kupata elimu ambayo itamsaidia mtu kupambana na mazingira yake na siyo kupata vyeti vya kuonyesha.
 
Hahahaaaa

Aisee unanichekesha sana ujue

Wewe kiwango maximum au minimum cha mwanadamu kuchukua maarifa kwenye ubongo wake hivi wewe umejulia wapi ndugu yangu?

Utueleze tu umetumia mashine gani kujua eti hii ni "maximum ya maarifa needed"?

Mkuu wewe umetumia ubongo wako uwezo wake binafsi ya kuhandle maarifa kutoa hii suggestion yako,hujafanya research popote kupima hili

Mkuu unatoa your own biased observations kutokana na mapafu ya ubongo wako kutawanya eti ni shida ya watoto wote nchini..

Hapana,stop this.

Unaona wewe umeona hayo uliyotaja yaondolewe,ukija kwangu nina list ingine tofauti kabisa ningependa yaondolewe,mwingine akija ana list yake...hii ni subjectivity,hakuna cha maana

Ni chaos tupu

Kwa kifupi soma yanayokuhusu,faulu ukifeli hatukutaki kwenye jamii tukukabidhi wagonjwa wetu uwafanyie operations au urushe ndege zetu,we will never trust you

Una option ya kuacha kusoma,ila tutakupa kazi zisizotumia ubongo,usitulaumu
Kipimo ni output.Graduate hawajaonesha kuwa hayo mambo mengi walio yasoma yana weza kuwakomboa.Nchi ni masikini, ufisadi,ubabaishaji,umangi meza, Teknolojia duni, uelewa mdogo wa mambo ya kimataifa,uzombi nk.Wew yote hayo huyaoni? Unataka kipimo gani? Hakuna innovation kubwa tuliofanya ambayo ina akisi utitiri wa mambo yanayofundishwa.Karne ya 21 madarasa hayana umeme wala madirisha, watoto hawali chakula asubuhi mpaka jioni.Watu wengi wamedhoofu kitafya na kiufahamu wapo wapo hawajui kwa nini wapo! unataka ushahidi gani tena.
Makundi ya vijana kukimbilia shughuli za boda boda, umachinga ,mama lishe na shugHuli zisizo eleweka kisa hawana ujuzi wa maana walioupata mashuleni wa kuwafaa matushani,unataka ushahidi gani au nawe umedumaa ubongo kutokana na kukosa lishe bora?
Mtu asubuhi anaamkia viazi/ mihogo na chai,mchana ugali na matembele na usiku wali maharage, huyo amesoma kweli? Mkuu maajabu ni mengi sana,Kama yote hayo huyaoni basi mkuu unashida kwenye medula yako.
 
Naonelea History na Civics ziwe hazina mitihani wala notisi. Zifundishwe kwa njia ya masimulizi. Tena ili kurahisisha ugumu masomo haya yasimuliwe kwa lugha ya Kiswahili.

Pia mtaala wa kiswahili upunguzwe. Mambo ya mofimu na kuchambua sentensi yatolewe na ikiwezekana kidato cha pili iwe mwisho kukisoma, anayetaka anaweza kuendelea nacho akifika kidato cha tano.

Mambo ya mofimu na vitenzi hayasaidii kitu maishani.

Naomba tujadili hili na nyinyi wakuu sana mtoe maoni yenu jinsi ya kumpunguzia mzigo mwanafunzi wa sekondari.
Nenda darasani kasome. Mchezo wa kuchezea simu vichakani haitakusaidia. Hata zamani topic hizo zilikuwepo na masomo hayo yalikuwepo. Usitafute urahisi. Tunataka wabobezi sio wasomi mlenda !!
 
Biolojia inatusaidia kujua mwili na afya zetu, fizikia ndiyo msingi wa ufundi, hesabu tunatumia kila siku. Chemistry, tunatumia kila siku kemikali jiografi na kiingereza ni muhimu sana.
Kwamba kiingereza kufundishwe Lin kiswahili hapana eti,hujui Kuna watu wanachukua degree za kiswahili? Sio Kila kitu ambacho siyo applicable kwako hakiapply kwa wengine,hi dunia ni kubwa kiswahili kinaendelea kukua wageni wengi wanaanza kujifunza kiswahili,walimu was kuwafundisha watatoka wapi Kama kimefutwa wizara ya elimu sio wajinga kuyaacha hayo masomo, history inafundishwa duniani kote su ulaya si Asia wanaujua thaman yake waache watoto wasomebana wape uwanja mpana wa kuchagua
 
Kwanza Mtihani ndiyo Nini, unamkuta mwanafunzi kaatamia Mtihani anaficha Ili mwenzake asimgeze (roho mbaya) ya waafrica ataki mwenzake apate,
 
Mkuu una hoja ya msingi mnoo...sema maccm ndo hivyo. Fikra finyu.
Masoma yanayohitajika kwa Sasa ni


1.mathematics
2.physics
3.geograph
4.biology
5.chemistry
6.economics
7.agriculture

ambayo yanahitaji modification

1.history and civics supposed to be one subject
2.kiswahili
3.language/English
4.kifaransa -lifutwe .
 
Kuwe na shule za ufundi... Kilimo... Science..
Kwishaaa.

Na kila level mtu akimaliza aweze kujiajiri.

Nasema kila siku li mtaala la mkoloni lilishapitwa na wakati.

Hovyo kaibisa.
 
Mimi yamenisaidia nashauri yawe masomo ya lazima toka shule ya msingi mbaka chuo kikuu.
 
Output umeipimia wapi?

Toa takwimu hapa au unahisi tu na ubongo wako wa kivivu?

Nani kakwambia ni mambo mengi?

Uki-compare na nini?

Wewe umetumia kipimo gani kujua ni mambo "mengi" na sio machache au wastani?

Takwimu za kukombolewa au kutokombolewa wewe umezipata wapi?

Maana nadhani unashindwa kuelewa madaktari wanaokutibu hospitali leo wamesoma hayo mambo mengi,ma-engineer wanaojenga hizo skyscappers na madaraja na barabara ndio hao hao waliosoma mambo mengi,maprofessors wanaofundisha wanao vyuoni ni hao hao walisoma mambo mengi,etc

Wewe ulitaka jinga kama wewe lisilojua chochote ndio likatibu hospitali?

Hujui lugha,hujui kuandika kwa ufasaha,wewe ni doctor utaweza waandikia wagonjwa dawa kwa usahihi?Au ndio unataka kuua watu?

Ni kosa la kua na uchumi mdogo na ukosefu wa serikali imara yenye kufanya kazi

Udhaifu wa serikali ndio ufanye elimu ichakachuliwe iwe nyepesi kukidhi upumbavu wa umasikini ulionao?

Hoja za kimaandazi sana hizi

Eti sababu mtoto hali shule,hakuna madawati,etc basi tupunguze masomo yawe mepesi kufidia umasikini huu,hiyo itakua elimu au group la manyani limekaa kusoma vitabu visivyo na maana?

Naona unachanganya issue mbili tofauti hapa

Umasikini na udhaifu wa kimaendeleo wa serikali na nchi yako na standard za elimu kama elimu...

Wewe unakuja na hoja za kipumbavu eti masomo yapunguzwe,hoja ulizonazo eti kwavile sisi masikini,kwahiyo upunguze elimu kufata umasikini wako chini?


Mwenye matatizo na medulla yake ni wewe hapo

Kwanza hujui kupangilia paragraph na kutofautisha hoja za kiuandishi kwa mafungu

Insha ulifundishwa wapi?Proof writting ulifundishwa wapi?

Halafu upo hapa kusema Kiswahili kifutwe,Historia ifutwe,nk?

Unafuta Kiswahili kama lugha,wewe una maarifa,utawezaje kuyaandika kwenye kitabu ili kizazi kifuatacho kifaidike kama hujui kuandika kwa usahihi na kupangilia mawazo yako na topics kwenye kitabu kwa usahihi na kwa lugha fasaha na sanifu?

Wewe ni engineer ila hujui yote hayo,utashindwa andika vitabu kuweka maarifa yako mle kwa ajili ya kizazi kijacho sababu tu hujui Wrting Skills,halafu upo hapa unasema yote haya yafutwe?

Tanzania ina mitoto mijinga mno,na wewe ni limoja lao,shule inakushinda unataka sukumizia ujinga wako kwa wengine wasiohusika na your own weaknesses

Wewe ni mvivu,hutaki juhudi,wewe feli ukaoshe vyoo,wenye juhudi ya kupata maarifa waje wakuongoze,na hoja yako ya kufuta eliu bad can never be
Mkuu umeandika vitabu vingapi?
Umefanya innovation gani?
Kwa nini unaamini mfumo uliopo upo sahihi iwapo huwezi onesha jambo la mfano ulilofanya au lililofanywa.
Hivi hujui kushindwa kupanga lishe inatokana na elimu duni! Kama jamii mnashindwa kuona umuhimu wa chakula shuleni hivi hicho kiswahili kina umuhimu gani kukisoma?
Skyscraper ndio kipimo cha ubora wa elimu kwako?
Je unaweza kuthibisha kuwa umasikini wa nchi na watu wetu hautokani na uduni wa elimu?
Udhaifu wa maendeleo wewe kwako si udhaifu uliotokana na elimu duni,.
Serikali inaendeshwa na nani kama sio raia waliozalishwa na mfumo huo wa elimu!
Hivi kushindwa kujenga madarasa ni mpaka muisubiri serikali kuu, huoni ni udumavu wa ubongo huo?
Unaonekana hata hujamuelewa mtoa mada unakurupuka tu kutukana, jenga hoja acha kutukana, watu wenye hoja dhaifu huishia kutukana ili kujihami.
 
Nenda darasani kasome. Mchezo wa kuchezea simu vichakani haitakusaidia. Hata zamani topic hizo zilikuwepo na masomo hayo yalikuwepo. Usitafute urahisi. Tunataka wabobezi sio wasomi mlenda !!
Ndiyo maana mnaelewa vitu nusunusu.
 
This time mwanafunzi atakoma tu anaweza jikuta kawa endangered sp kama huyo kiumbe kwenye avatar
 
Back
Top Bottom