Mwanafunzi wa Shule ya Msingi aua mwenzake kwa ngumi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ilola, Kata ya Ilola Itwangi, Wilaya ya Shinyanga Vijijini, mkoani hapa, mwenye umri umri wa miaka 12 (jina lake linahifadhiwa kutokana na umri wake), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mwenzake kwa kumpiga ngumi kichwani na kuangukia kisogo, wakati wakigombea daftari waliloazima.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Longinus Tibishubwamu, jana alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 7:30 mchana na kwamba, wanamshikilia mwanafunzi huyo kwa mahojiano na kwamba wakikamilisha upelelezi atafikishwa mahakamani.

Alimtaja mwanafunzi aliyefariki dunia kuwa ni Veronica Venance (12), aliyekuwa anasoma darasa moja na mwezake aliyesababisha kifo hicho.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Magere Jonas, alisema wakati wanafunzi hao wanagombea daftari hilo, alikuwa amepumzika chini ya mti akiwa na mwalimu mkuu msaidizi.

Alisema ghafla walipelekewa taarifa kuwa kuna wanafunzi wanagombana darasani.

Jonas alisema baada ya kuingia darasani, walimkuta mwanafunzi huyo akiwa amelala chini akigalagala, hivyo kumkimbiza kwenye kituo cha afya Bugisi kilichoko jirani na shule hiyo, lakini kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo alifariki dunia.

Mtendaji wa Kata ya Ilola, Mahona Joseph, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza marehemu alikuwa ameng'anga'nia daftari alilokuwa ameazimwa na Sophia Mathew kwa ajili ya kuandika ‘notes' kitendo ambacho kilimkera mwenzake na kuzua ugomvi.

"Tunahisi kifo cha mwanafunzi huyu kilitokana na kuanguka vibaya mara baada ya kusukumiwa ngumi na kukipiga kisogo, hivyo kukata mawasiliano na kusababisha kifo chake. Masuala mengi tumeviachia vyombo vya maamuzi," alisema Joseph.


Chanzo:
Nipashe
 
Sophia na Mwalimu wa somo husika nao wakamatwe.
 
Kama lulu tu anapeta mtahani itakuwa huyu wa darasa la 6. Mambo mengine wazazi wakae yaishe. Dogo arudi shule tena ikibidi haamishwe na shule. Pia waangalie record ya dogo kwa tabia zake kama itakuwa ndo ataendelea basi wakapeleke rumande tu . Ila hapo ni kifo cha kutokusudia maana ugomvi wa madogo upo sana mashuleni na mitahani.
 
Unauhakika kwamba notes zilitolewa kwa mtindo huo?

How if hao w'funzi walikua watoro?

What if utoro ulikuwa na genuine excuse, kama huyo aliyefiriki, what is hakuwa akihudhuria darasani kutokana na kusumbuliwa na maradhi?

au ndo utasema basi na ma CCM yakamatwe kwa kushindwa kuboresha huduma za afya?
 
What if utoro ulikuwa na genuine excuse, kama huyo aliyefiriki, what is hakuwa akihudhuria darasani kutokana na kusumbuliwa na maradhi?

au ndo utasema basi na ma CCM yakamatwe kwa kushindwa kuboresha huduma za afya?

My point is: Hizi burden tunazowabebesha walimu kwa kesi kama hizi (hope ni hii tu) sizo na hazijengi.

Mwalimu atasimamia hivyo w'funzi wangapi? anafundisha madarasa mangapi? Anakazi ngapi?

Point yako ni kwamba walimu ni wazembe (ikiwa nikekuelewa) Jee unaweza kuelezea uzembe wa mwalimu hapo?
 

Point yangu ni kwamba ma CCM yamevuruga mfumo wa elimu nchini, hakuna walimu wa kutosha kuwezesha kila mwanafunzi kupata support ya kutosha kutoka kwa walimu.

habari hii inaonyesha madhara ya mfumo mbovu wa elimu sio tu yanasababisha kuwa na Taifa la wajinga bali vifo kwa wanafunzi pia?
 
Ngumi moja tuu adi anauwa??? .....Daa huyo dogo atakuja kuwa bondia wa hatareee kweli kweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…