TANZIA Mwanafunzi wa UDSM (COET) agongwa na gari

TANZIA Mwanafunzi wa UDSM (COET) agongwa na gari

Habari hii inagusa sana, sijui ni kwa vile mwandishi ana uelewa wa kuandika.
Poleni sana na kwa wale wanaoelewa COET alumni mwaka wa nne wanajua hicho kichwa kimoja kilikuwa na uzito gani kuanzia marafiki, familia hadi taifa!

Lakini hapa tukumbushane suala la msingi; watu wengi Tanzania hasa Dar es Salaam waliopewa leseni za kuendesha magari, kumilikishwa siraha za moto, madaraka ya kuamua nk ni watu ambao hawakustahili na ndio maana hata uendeshaji wa magari ni wa kuuana uana!
 
Jamani tuone umuhimu wa kuwa na na ambulance na namba za dharura ka ilivyo zima moto. Miaka 50 ya Uhuru bado tunaishi ka nyumbu. Boda boda wengi wanagongwa na kukaa barabarani kwa muda murefu tukisubiri wasamalia wema hii sio sawa . Napongeza wabunge wanaojitolea ambulance. Poleni sana.
 
duh..mtu mzima machozi yamenitoka kwa kijana mwenye matumaini kupoteza maisha yake. Bila shaka ni matokeo ya uzembe na ufisadi uliokithiri kwenye jamii yetu. Mungu amrehemu roho yake.
 
RIP mwanafunzi,lakini nimejigundisha kitu,siku hizi watu wanaogopa kusimama na kutoa msaada maana hii pia ni mbinu ya vibaka kukupiga roba,lakini pia polisi wasumbufu,watataka ukae nao hadi ukaandike maelezo,wakuhoji kana kwamba ww ndio umegonga
 
Poleni sana MUNGU awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu!! RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA....................... APUMZIKE KWA AMANI!!
 
RIP
Watz tuna tabia ya kupita ajali pasipo kutoa msaada.
Itatokea siku utampita nduguyo wa karibu na akapoteza maisha kwa kukosa msaada wa haraka

Niliwahi kukuta ajali kama hii. Niliposimama kutoa msaada nilijuta maana nilitukanwa kwa niaba ya madereva wote. Na kibaya zaidi nilipofika hospitali polisi walinianzishia maelezo kama mimi ndio nimegonga. Kwa kifupi nilipata usumbufu sana. Ilikuwa nifike nyumbani saa 12 jioni nilifika saa 6 usiku na gari limetapakaa damu. Ni vizuri kutumia tuu magari ya polisi.
 
unajua nini?
Kwa jiji la dar
si chini ya watu kumi daily hupoteza maisha kwa ajali barabarani.
Ukiona zimetangazwa................ Ni kama hiiii
kama angekuwa mbangaizaji tyu,chinga ma ntili au teja.....
 
Huo ndo ulimwengu tunaoishi ambao watu wanajipenda wenyewe. vitabu vya mwandishi mmoja Ellen G white ameandika yote hayo. MATUKIO SIKU ZA MWISHO! Mungu awatie nguvu na matumaini, huyo kamaliza safari yake Je wewe na mimi tutamalizaje tumejiandaaa? tutapata muda wa kutubu?
 
RIP kwa ndugu yetu.

Lakini klifo cha huyu mwanafunzi na wengine wengi wanaogongwa ni matokeo ya mabo kadhaa kwenye jamii yetu
1.kujichukulia sheria mkononi pindi mtu akigongwa,hii imesababisha dereva akigonga mtu anakimbia eneo la tukio,na katika kukimbia ndio anamburuza aliemgonga hadi kumuua.
2.usumbufu wa polisi iwapo utajitolea kumsaidia aliegongwa,waliojitolea wanajua kadhia hii. na ndio maana kila gari mlilolisimamisha wakagoma.
4.uozo wa serikali na jeshi lake la polisi,wanachelewa kuja kwenye matukio kama haya ila ni wa kwanza kufika kupiga mabomu wanafunzi wakigoma. pia hamna hata ambulance hapa hapa mjini je huko vijijini??!
 
r.i.p kijana wetu

mtoa mada umefanya jambo jema kutoa funzo ya kwamba tuwe tunatembea na vitambulisho popote,nami naongezea funzo lingine,wakati wa kuvuka barabara kunapokuwa na magari machache ni hatari zaidi maana magari huenda kasi zaidi na inapokuwa ni usiku hali huwa mbaya zaidi,tuongeze tahadhari zaidi ktk mazingira hayo tajwa

lakini mwisho wa maelezo yako binafsi sijayapenda

kwanini umetengeneza "roho" ya kisasi???kusoma kwako hadi chuo kikuu kunakufanya uamini dereva anaweza kufanya makusudi kumgonga mtu???na hata wa gari la pili na la tatu unaona nao wamefanya makusudi kumgonga?

Sio roho ya kisasi, nadhani hujaelewa ni jinsi gani tukio hili linavyosikitisha na kutia hasira. Kwamba inawezekana kulikuwa na uwezekano wa kijana kupona kama kila mtu angewajibika haraka iwezekanavyo. Huyo dereva baada ya kukimbia (kuhofia maisha yake - saa nyingine inabidi tu) angejisalimisha polisi na wakaja fasta. Halafu tunaambiwa tuwe tunapiga namba ya polisi kupata msaada. Angalia response yao sasa. Afrika vinatokea vifo vingi vya kizembe, kimaskini na kwa ajili ya wapumbavu wachache, sasa tukiendelea kutoonyesha hisia zetu na kuchukua hatua unafikiri mambo yatabadilika?
 
Back
Top Bottom