Pangaea
JF-Expert Member
- Jun 14, 2012
- 202
- 41
Poleni walimu. Ila matatizo haya huwa mnajitakia wenyewe, yaani nyie kila mwaka wa uchaguzi hamkomi kutumiwa katika kampeni halafu mnaachwa huku mkiamini mambo yatabadilika. Tokea 1995, 2000,2005 and 2010, hamchoki tu!
Mko wengi na mna ushawishi katika jamii kama mkitumia nafasi zenu vizuri.
Kumbukeni, mliyempigia kura mara mbili ameshawaambia hayo madai yenu hayawezekani kabisaaaaaa!
Amkeni bana!
Nijuavyo walimu wengi wana mawazo huru na si rahisi kutumika. Hata hivyo katika kundi kubwa kama hili tutarajie si rahisi wote kuunga mkono wazo na mtizamo mmoja. Jamani tuendelee kuwaelimisha wale ambao bado hawajabadilika.