Mwanafunzi, weka swali linalokusumbua ili walimu na wazoefu wakusaidie

Mwanafunzi, weka swali linalokusumbua ili walimu na wazoefu wakusaidie

Umri wa Asha ni mara tatu ya umri wa Idd sasa. Miaka 5 iliyopita jumla ya umri wao ulikuwa miaka 14. Tafuta umri wa asha miaka 5 iliyopita.

Umri wa sasa wa Sadiki ni robo ya umri wa baba yake. Baada ya miaka 3 umri wa Sadiki utakuwa theluthi ya umri wa baba yake kwa wakati huo. Tafuta umri wa sasa wa baba yake.

Umri wa Tuli ni mdogo kuliko Nuru kwa miaka 6. Ikiwa jumla ya umri wao ni miaka 24,nini umri wa Nuru?

Wakuu naombeni msaada wa njia za kukukotoa maswali hayo
 
Umri wa asha ni mara tatu ya umri wa idd sasa.Miaka 5 iliyopita jumla ya umri wao ulikuwa miaka 14.Tafuta umri wa asha miaka 5 iliyopita.
Umri wa sasa wa sadiki ni robo ya umri wa baba yake.Baada ya miaka 3 umri wa sadiki utakuwa theluthi ya umri wa baba yake kwa wakati huo.Tafuta umri wa sasa wa baba yake.
Umri wa tuli ni mdogo kuliko nuru kwa miaka 6.Ikiwa jumla ya umri wao ni miaka 24,nini umri wa nuru?
Wakuu naombeni msaada wa njia za kukukotoa maswali hayo


Watafute uwaulize umri wao, watakwambia.

By the way, si vizuri kuingilia mambo ya familia fulani.
 
Hesabu za algebra za darasa la tano. Nitakupa majibu tuu. Njia ya kukokotoa ni vyema uumize kuchwa.

1.Umri wa Asha miaka mitano iliyopita ulikuwa na miaka 13.
2.Umri wa baba yake Sadiki miaka mitatu ijayo utakuwa miaka 27
3.Nuru ana miaka 15.
 
Mkuu JMF please naomba msaada wako unioneshee japo njia kwa hesabu moja namna ulivyokokotoa ili niweze kuzikumbuka
 
Hesabu za algebra za darasa la tano. Nitakupa njia tu. majibu yametolewa
umri wa idd = x, umri wa asha = 3x; miaka 5 iliyopita : (3x-5)+(x-5)=14 kwa hivyo x=6

umri wa baba= p, umri wa sadiki = 1/4 p; miaka 3 ijayo : 3(1/4p+3) = (p+3) kwa hivyo p=6

umri wa nuru = k, umri wa tuli = k-6; (k-6)+k=24 kwa hivyo k=15
 
Mkuu JMF please naomba msaada wako unioneshee japo njia kwa hesabu moja namna ulivyokokotoa ili niweze kuzikumbuka
A= umri wa Asha
I= umri wa Iddi

Sasa hivi 3×I=A,
miaka mitano iliyopita,
(3I-5)+(I-5)=14
4I-10=14
4I=14+10
4I=24
I=6, umri wa Iddi sasa, 6×3=18,umri wa Asha sasa.
Umri wa Asha miaka mitsno iliyopita ni 13
 
Ahsanteni nyote mlionipa muongozo wa kuzikokotoa hizo hesabu za umri.Mbarikiwe sana
 
Vipi mkuu ni ticha wa shule ya msingi nin au dogo homr kakuletea maswali yamekupiga vibaiskeli.!!?
 
Kama umeelewa hilo hebu jaribu ili nione kama umeelewa kweli. Samahani swali lipo kwa kizungu:
A car and a van started at the same time from town P and travelled towards town Q at a constant speeds. The speed of the car was 40 km/hr faster than the speed of the van. After 6 hours, the car reached town Q while the van had only completed 3/5 of the journey. Find the speed of the car.
 
Chemsha Bongo zenu zinazoelekea kulala:
Nimepanga viti kwenye ukumbi katika mistari 15 kwa ajili ya mkutano. Baada ya kikao naagiza wahudumu watoe viti 6 na kupanga viti vinavyobaki katika mistari 12 kwa ajili ya Kikao cha Kamari ya Harusi, matokeo yake imeongezeka mistari 9 katika mpangilio huu mpya. Niambie, kuna viti vingapi katika mpagilio huu wa kikao cha harusi?
 
Wakuu katika kupitia nyuzi mbalimbali humu nimegundua hili jukwaa lina wanafunzi wengi sana hasa kidato cha 5 au chini ya hapo pia wanavyuo

Hivyo basi ni vyema walimu na watu wenye uzoefu tuwasaidie hawa watu ili wafanye vyema ktk masomo yao kwa wenye nia njema, jukwaa hili ni muhimu na tukilitumia tukainua ufaulu wa ndugu zetu tutaongeza Tanzania njema yenye wasomi bora.

karibuni, mimi tupia swali la linguistics/language 1&2 (kwa A-level) au english kwa O - level na Geography.

Walimu wazuri na Wataalam wengine watajitajitokeza ukirusha swali lolote
teacher ni kozi ipi ya nzuri ya uhandisi naomba kama unaweza pia nielezee kwa list
 
.]
 

Attachments

  • 1472377777848.jpg
    1472377777848.jpg
    12.4 KB · Views: 75
Mtu aliyemaliza degree ya ualimu ana qualify kusoma
M. A Business Admnistration ?
 
MSAADA TAFADHALI; 1.TAJA NJIA TANO ZA KUWASILISHA MATOKEO AU ALAMA ZA MTIHANI
2.Taja vigezo vya kurekebisha alama au matokeo
 
Back
Top Bottom