Mwanahabari wa Citizen TV, Francis Odee, alikamatwa na maafisa wa polisi Jumanne, Oktoba 20, 2026, alipokuwa akiripoti maandamano ya wananchi waliokuwa wakipinga ongezeko la bei za mafuta katikati mwa jiji la Nairobi.
Odee, ambaye huripoti masuala ya uhalifu na usalama, alikuwa akitekeleza majukumu yake katika Barabara ya Kimathi wakati maafisa wa polisi waliovalia kiraia walipomkamata na kumlazimisha kuingia kwenye gari la polisi.
Video zilizosambaa mitandaoni zilionyesha maafisa hao wakimburuta mwanahabari huyo karibu na makutano ya Barabara ya Kimathi na Kenyatta Avenue, licha ya wananchi na wanahabari wengine kuwaeleza kuwa alikuwa kazini.
Akizungumza baada ya kuachiliwa, Odee alidai kuwa alijitambulisha kama mwanahabari lakini maafisa hao hawakumsikiliza. Alisema alisukumwa, kubanwa na kuchanwa nguo wakati wa kukamatwa kwake.
Alieleza kuwa alihofia maisha yake alipofikishwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Nairobi, akirejelea kifo cha mwalimu na mwanablogu Albert Ojwang, aliyefariki akiwa kizuizini katika kituo hicho.
Mwanahabari huyo aliachiliwa baadaye siku hiyo baada ya kuingilia kati kwa maafisa wakuu wa polisi.
Kukamatwa kwake kulijiri wakati wanaharakati wakiandamana kupinga bei mpya za mafuta zilizotangazwa na Mamlaka ya Kudhibiti Nishati na Petroli (EPRA), ambapo petroli iliongezeka kwa KSh12.93 kwa lita, dizeli KSh9.90 na mafuta ya taa KSh28.49.
Baraza la Vyombo vya Habari nchini (MCK) na Chama cha Wahariri Kenya (KEG) vimelaani tukio hilo, vikisema kukamatwa na kudhulumiwa kwa mwanahabari anayetekeleza majukumu yake kunahatarisha uhuru wa vyombo vya habari.
Mashirika hayo yamemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi, Douglas Kanja, kuhakikisha tukio hilo linachunguzwa na maafisa waliohusika wanawajibishwa iwapo watabainika kukiuka sheria.
Hata hivyo, kufikia wakati wa taarifa hizo, polisi hawakuwa wametoa maelezo rasmi kuhusu sababu za kumkamata Odee.
Source: Citizen TV