Mwanahalisi: JK apora nyumba Dar, mwenyewe aja juu

Mwanahalisi: JK apora nyumba Dar, mwenyewe aja juu

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
Nyumba ya Kikwete yazua utata

Rais Jakaya Kikwete anatuhumiwa kuchukuwa nyumba ya mkazi mmoja wa dare s Salaam na kuigeuza yake, MwanaHALISI limeelezwa.

Nyumba hiyo iko kiwanja namba 64, chenye eneo la futi mraba 23,239 kwenye makutano ya barabara ya Ursino na Migombani eneo la Mikocheni, Das es Salaam.

Hii ni nyumba ambamo wamekuwa wakikaa maofisa wa ngazi za juu serikalini, lakini warithi wanadai Kikwete ameibomoa, kijenga upya na ‘kujimilikisha.’

Nyumba hii, kwa mujibu wa warithi ni mali ya Amiral Abdulrasul Alarakhia Dewji na Yusufali Kassamali Remtula Parpia, ambao wote ni marehemu.

Mmoja wa warithi ni Amiral Yusufal Parpia ambaye anawakilishwa na kampuni ya mawakili ya H.H. Mtanga & Co Advocates ya Dar es Salaam.

Kwa kuwa nyumba hii imekuwa ikikaliwa na maofisa wa serikali, na kwa kuwa sechi kuhusi mmiliki wa kiwanja ya 22 Julai 2002 bado inaonyesha kuwa wamiliki ni wale wale, warithi wanapanga kuifikisha serikali mahakamani kwa kubomoa nyumba yao.

Tayari mawakili wa warithi wameitaarifu serikali kuhusu kusudio la kuifikisha mahakamani wakati wowote kujibu madai ya wateja wao………….

……….Hivi sasa Rais kikwete na familia yake wanaishi Ikulu, Magogoni. Lakini kabla ya kupata madaraka ya urais mwaka 2005, alikuwa akiishi katika nyumba hiyo kwa takriban miak 15 akiwa kama mtumishi wa serikali.

Hata sechi ya awali ya kiwanja hicho ya 22 Agosti 1982 iliwataja wamiliki kuwa hao hao, Dwewji na Parpoia.

Bali sechi nyingine ya wizara juu ya kiwanja hicho hicho ya 5 Novemba 2010 inasema, pamoja na mamobo mengine, kuwa imeshindikana kupata rekodi zinazoonyesha mmiliki wa kiwanja hicho……

Habari zaidi katika MwanaHalisi.

My Take:
Huu ni unyang’anyi wa hali ya juu. Hata hivyo hii habari iliwahi kutoka huko nyuma katika miezi ya awali ya utawala wa JK ingawa siyo katika details nyingi kama hivi.

Nyumba ya Kikwete yazua utata

Rais Jakaya Kikwete anatuhumiwa kuchukuwa nyumba ya mkazi mmoja wa dare s Salaam na kuigeuza yake, MwanaHALISI limeelezwa.

Nyumba hiyo iko kiwanja namba 64, chenye eneo la futi mraba 23,239 kwenye makutano ya barabara ya Ursino na Migombani eneo la Mikocheni, Das es Salaam.

Hii ni nyumba ambamo wamekuwa wakikaa maofisa wa ngazi za juu serikalini, lakini warithi wanadai Kikwete ameibomoa, kijenga upya na ‘kujimilikisha.'

Nyumba hii, kwa mujibu wa warithi ni mali ya Amiral Abdulrasul Alarakhia Dewji na Yusufali Kassamali Remtula Parpia, ambao wote ni marehemu.

Mmoja wa warithi ni Amiral Yusufal Parpia ambaye anawakilishwa na kampuni ya mawakili ya H.H. Mtanga & Co Advocates ya Dar es Salaam.

Kwa kuwa nyumba hii imekuwa ikikaliwa na maofisa wa serikali, na kwa kuwa sechi kuhusi mmiliki wa kiwanja ya 22 Julai 2002 bado inaonyesha kuwa wamiliki ni wale wale, warithi wanapanga kuifikisha serikali mahakamani kwa kubomoa nyumba yao.

Tayari mawakili wa warithi wameitaarifu serikali kuhusu kusudio la kuifikisha mahakamani wakati wowote kujibu madai ya wateja wao………….

……….Hivi sasa Rais kikwete na familia yake wanaishi Ikulu, Magogoni. Lakini kabla ya kupata madaraka ya urais mwaka 2005, alikuwa akiishi katika nyumba hiyo kwa takriban miak 15 akiwa kama mtumishi wa serikali.

Hata sechi ya awali ya kiwanja hicho ya 22 Agosti 1982 iliwataja wamiliki kuwa hao hao, Dwewji na Parpoia.

Bali sechi nyingine ya wizara juu ya kiwanja hicho hicho ya 5 Novemba 2010 inasema, pamoja na mamobo mengine, kuwa imeshindikana kupata rekodi zinazoonyesha mmiliki wa kiwanja hicho……

Habari zaidi katika MwanaHalisi.

My Take:
Huu ni unyang'anyi wa hali ya juu. Hata hivyo hii habari iliwahi kutoka huko nyuma katika miezi ya awali ya utawala wa JK ingawa siyo katika details nyingi kama hivi.

Ningekuwa mimi ningetoka mkuku, ile ya msoga mie inanitosha:happy:
 
duuu hii kali rais anayejiita "mtu wa watu" ...kapora nyumba ya yatima........so bad..

hii imemkalia pabaya ..huyu ndio JK ambayee wakati wa kampeni za ndani ya chama early 2005 alikuwa akijipambanua kama mpingaji wa kuuza nyumba za serikali.....kumbe alikuwa akiishi nyumba ya yatima ..na akaamua kujitualia...akidhani nayo ni ya serikali..

Wanasheria wa serikali wamshauri rais amalizani nao haraka ..kwa pesa yake ...maana hili halikwepeki..kama yeye anavosema kuwalipa dowans haikwepeki!
 
maskini duh,anyway ndo hivo ishaenda tena
 
Hakuna kilicho nafuu kuiba hata kimoja, licha ya mke wa mtu hata kuiba mtumishi wa mtu haitakiwi! Ni dhambi!
 
Lakini rais si ana mamlaka ya kubadilisha au kubatilisha matumizi ya hati au ardhi yoyote ndani ya taifa lake? Ningekuwa mkulu ningetamka, "tangu tarehe...kwa mamlaka nliyopewa na katiba ya JmT nimebatilisha hati no...ya mwaka...Tangu hapo itakuwa mali ya rais aliye kwenye utamu,no kwenye atamu". Alaf natulia magogon nichek nani atapanua domo. Teeh teeh teeh! Mkulu bwn,iyo ndo akili ya k uambiwa mkulu...
 
Aliwahi kupora viwanja Mwanza,pande za Nyegezi.................
 
Nafuu kuiba mke wa mtu kuliko kuiba nyumba ya yatima.
Mkuu,
Hapana!
Mke wa mtu unauwawa, lakini kwa kesi hii mtaendeshana hata kwa miaka 10.
Ila useme uwezekano wa hawa wadai kupata nyumba hii ni mdogo...watasumbuliwa sana hata na Usalama/Uadui wa Taifa, na mwishowe mzee akilala vizuri anaweza kuwapa kiwanja huko M'BWEWE!
 
kumbe nyumba yenyewe ya wahindi?kwani kikwete akistaafu hataki kukaa kijijini?aghhh
 
Kama hii nyumba ilikuwa ya serikali kama nyumba nyingine ambazo watumishi wa serikali walikuwa wanakaa, na baadae hao watumishi wa serikali wakaamua kujiuzia wakati Magufuri akiwa waziri wa ujenzi, iweje nyumba ambayo kikwete alinunua na ilikuwa ya serikali leo hii iwe ya wahindi walio marehemu??????????/
 
tusubirie iende mahakani kwanza...ingawa chance ya kuipata ni ndogo
 
nchi inaelekea wapi hii!! kila kukicha ni kashfa juu ya kashfa..kama ni kweli presdaa inabidi arudishe mjengo huo.
 
Kama hii nyumba ilikuwa ya serikali kama nyumba nyingine ambazo watumishi wa serikali walikuwa wanakaa, na baadae hao watumishi wa serikali wakaamua kujiuzia wakati Magufuri akiwa waziri wa ujenzi, iweje nyumba ambayo kikwete alinunua na ilikuwa ya serikali leo hii iwe ya wahindi walio marehemu??????????/

Hakuna mahali gazeti la MwanaHalisi limesema nyumba hiyo ilikuwa ni mali ya serikali. gazeti limesema tu kwamba ilikuwa inakaliwa na wafanyakazi wa serikali -- yumkini kwa maana ya serikali kupangisha kwa ajili ya wafanyakazi wake.

Au kuna mtu kaelewa vingine?
 
Kwani hao wamiliki wa hiyo nyumba waliipangisha serikali au walimpangisha JK?
 
Kila nikiamka asubuhi nadhani hata ntasikia zuri lolote la hii serikali lakini naambulia pressure na depression,yaani sielewi
 
Nyumba waliuza wenyewe kwa nei ya kutupa,tena waliuziana,leo wanzigeukia za wananch
 
Back
Top Bottom