Nyumba ya Kikwete yazua utata
Rais Jakaya Kikwete anatuhumiwa kuchukuwa nyumba ya mkazi mmoja wa dare s Salaam na kuigeuza yake, MwanaHALISI limeelezwa.
Nyumba hiyo iko kiwanja namba 64, chenye eneo la futi mraba 23,239 kwenye makutano ya barabara ya Ursino na Migombani eneo la Mikocheni, Das es Salaam.
Hii ni nyumba ambamo wamekuwa wakikaa maofisa wa ngazi za juu serikalini, lakini warithi wanadai Kikwete ameibomoa, kijenga upya na kujimilikisha.
Nyumba hii, kwa mujibu wa warithi ni mali ya Amiral Abdulrasul Alarakhia Dewji na Yusufali Kassamali Remtula Parpia, ambao wote ni marehemu.
Mmoja wa warithi ni Amiral Yusufal Parpia ambaye anawakilishwa na kampuni ya mawakili ya H.H. Mtanga & Co Advocates ya Dar es Salaam.
Kwa kuwa nyumba hii imekuwa ikikaliwa na maofisa wa serikali, na kwa kuwa sechi kuhusi mmiliki wa kiwanja ya 22 Julai 2002 bado inaonyesha kuwa wamiliki ni wale wale, warithi wanapanga kuifikisha serikali mahakamani kwa kubomoa nyumba yao.
Tayari mawakili wa warithi wameitaarifu serikali kuhusu kusudio la kuifikisha mahakamani wakati wowote kujibu madai ya wateja wao
.
.Hivi sasa Rais kikwete na familia yake wanaishi Ikulu, Magogoni. Lakini kabla ya kupata madaraka ya urais mwaka 2005, alikuwa akiishi katika nyumba hiyo kwa takriban miak 15 akiwa kama mtumishi wa serikali.
Hata sechi ya awali ya kiwanja hicho ya 22 Agosti 1982 iliwataja wamiliki kuwa hao hao, Dwewji na Parpoia.
Bali sechi nyingine ya wizara juu ya kiwanja hicho hicho ya 5 Novemba 2010 inasema, pamoja na mamobo mengine, kuwa imeshindikana kupata rekodi zinazoonyesha mmiliki wa kiwanja hicho
Habari zaidi katika MwanaHalisi.
My Take:
Huu ni unyanganyi wa hali ya juu. Hata hivyo hii habari iliwahi kutoka huko nyuma katika miezi ya awali ya utawala wa JK ingawa siyo katika details nyingi kama hivi.