PreGE2025 Mwanaharakati wa haki za Binadamu Agather Atuhaire, apatikana baada ya kutupwa mpaka wa Tanzania-Uganda, Mtukula

PreGE2025 Mwanaharakati wa haki za Binadamu Agather Atuhaire, apatikana baada ya kutupwa mpaka wa Tanzania-Uganda, Mtukula

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Yaani mtu anashabikia serikali iliyounda kikosi cha kubaka watuhumiwa; kumbuka kuwa uzao wako siyo wote watakuwa na mawazo sawa na yako ya kushabikia unyanyasaji wa raia bali kuna wengine watabakwa kama hao unawashabikia leo hii.
Kikosi kinabaka gizani mnawashabikia, then wataanza kubaka raia adharani na hapo ndipo hadi watoto wa wabakaji nao watabakwa.

Muosha uoshwa.
Malipo ni hapahapa Duniani!
 
Acha wenge,wewe uzao wako utakqa wanaharakati wa kuvuruga amani
Hapana..

Haina shaka yoyote kuwa aidha huelewi kabisa dhana nzima ya uanaharakati (activism) au unaelewa lakini kwa makusudi umeamua mwenyewe kujichimbia kwenye dhambi ya "unafiki" wa kupotosha kwa makusudi jambo unalolijua kwa manufaa yako binafsi na hivyo kujichimbia kwenye dhambi nyingine ya "ubinafsi..."

Kwa mujibu OXFORD DICTIONARY...

Activism - is the act of the use of vigorous campaigning to bring about political or social change.

An activist - is someone who is active in campaigning for change, normally on political or social issues...

#Ndo kusema kila mwanasiasa ni activists

#Kila aliyemo humu ni activist

TOFAUTI ya activist huyu na yule ni aina ya mabadiliko ambayo kila mwanaharakati anayapigania..

Mfano:
• Nyie huko CCM na wanaowaunga mkono ni Wanaharakati pia mnaopambana kwa kampeni za kila namna kupigana kuzuia mabadiliko yoyote yenye kutaka kuipoka "Status quo" manufaa inayoyapata kupitia mifumo ya kisiasa na kiuchumi mibaya, kandamizi na isiyo haki katika jamii yenye kuwanufaisha ninyi wachache tu na si jamii yote kwa upana wake..

• Kwa upande wa pili wapo Wanaharakati wanaopigania mifumo chanya na bora ya kisiasa na kiuchumi hapa nchini Ili kuinufaisha jamii yote kwa mapana yake. Hawa ndiyo kina sisi, Agatha Atuhaire, Boniface Mwangi na Watanzania wengine kwa mamilioni ndani na nje ya nchi tukiongozwa na Tundu Lissu chini ya kaulimbiu ya NO REFORMS NO ELECTION..

Kwa hiyo, hebu acheni unafiki wa kujipotosha na kupotosha wengine..

Kama mmewapiga na kuwaumiza hawa raia wa kigeni, basi ni kwa sababu zenu mnazozijua wenyewe. Na kwa kweli, ni kwa kuwa tu upande wenu wa harakati zenu umeelemewa, hauwezi kujibu hoja kwa hoja badala yake mmeamua kujibu hoja kwa bunduki, kuteka, kuua kwa kuwa tu Watanzania wamewaoa dhamana ya kumiliki na kuzitumia hizo bunduki...

That's barbaric..!!
 
Hatimaye wasiojulikana wamevua mask, sasa ni hadharani. Uzuri wa dunia uko hivi, kila mtu atalipwa kwa mabaya yake anayoyafanya kwa uwazi ama sirini.

Damu za watu huwa haziendi bure. Mateso na kunyanyaswa vyote, huwa vina mwisho. Kwa Imani yako muombe Mungu, yeye hutenda na hufanya njia pasipo na njia.
 
Masaka, Uganda Kituo cha Utafiti cha Agora kimethibitisha kuwa mkurugenzi wao, Agather Atuhaire, ambaye tangu Jumatatu anashikiliwa na maafisa wa Tanzania, amepatikana asubuhi ya leo akiwa hai katika mpaka wa Uganda na Tanzania.

katika taarifa hiyo wameelezea kuwa "Tunafarijika kuufahamisha umma kuwa amepatikana. Alitelekezwa mpakani na mamlaka ya Tanzania. Maelezo zaidi yatatolewa baadaye leo. Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kila mtu ambaye alisimama kwa mshikamano wakati huu. Juhudi zako zilifanya mabadiliko," alisema Agora katika taarifa yake asubuhi ya leo.

Atuhaire alikamatwa pamoja na wanaharakati wengine waliokuwa wamesafiri hadi Tanzania kushuhudia kesi ya kiongozi wa upinzani Tanzania Tundu Lissu.

Agather Atuhaire ni mwanasheria wa Uganda, mwanahabari, na mwanaharakati wa haki za kijamii. Yeye ni mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Utafiti cha Agora.

Anajulikana kwa kazi yake kuhusu masuala kama vile rushwa, haki za binadamu na utawala bora na ametambuliwa kimataifa kwa uanaharakati wake. Kazi yake ni pamoja na kutetea ushiriki wa raia, mageuzi, na mabadiliko ya sera nchini Uganda. Mnamo 2024, alitunukiwa Tuzo la Kimataifa la Wanawake wa Ujasiri na Idara ya Jimbo la Merika.

Source: The Independent

Pia soma
Hawajamniniiihu.. .
 
Mara nyingi haya mambo yanapotokea najiuliza sana kuhusu uwepo wa Mungu. Je kama kweli yupo mbona kuna mambo mengi yanaendelea na hakuna mtu anaeweza kuhoji,ina maana Mungu hayaoni?
 
Masaka, Uganda Kituo cha Utafiti cha Agora kimethibitisha kuwa mkurugenzi wao, Agather Atuhaire, ambaye tangu Jumatatu anashikiliwa na maafisa wa Tanzania, amepatikana asubuhi ya leo akiwa hai katika mpaka wa Uganda na Tanzania.

katika taarifa hiyo wameelezea kuwa "Tunafarijika kuufahamisha umma kuwa amepatikana. Alitelekezwa mpakani na mamlaka ya Tanzania. Maelezo zaidi yatatolewa baadaye leo. Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kila mtu ambaye alisimama kwa mshikamano wakati huu. Juhudi zako zilifanya mabadiliko," alisema Agora katika taarifa yake asubuhi ya leo.

Atuhaire alikamatwa pamoja na wanaharakati wengine waliokuwa wamesafiri hadi Tanzania kushuhudia kesi ya kiongozi wa upinzani Tanzania Tundu Lissu.

Agather Atuhaire ni mwanasheria wa Uganda, mwanahabari, na mwanaharakati wa haki za kijamii. Yeye ni mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Utafiti cha Agora.

Anajulikana kwa kazi yake kuhusu masuala kama vile rushwa, haki za binadamu na utawala bora na ametambuliwa kimataifa kwa uanaharakati wake. Kazi yake ni pamoja na kutetea ushiriki wa raia, mageuzi, na mabadiliko ya sera nchini Uganda. Mnamo 2024, alitunukiwa Tuzo la Kimataifa la Wanawake wa Ujasiri na Idara ya Jimbo la Merika.

Source: The Independent

Pia soma

Hizi ni kesi za ICC, na wanaofanya wanafanya makusudi kumuharibia mama ila mama mwenyewe hajastuka bado
Yes, matukio haya ya Uhalifu mbaya Sana dhidi ya binadamu yanakidhi Vigezo vya Kimataifa vya Watawala kuweza kushitakiwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu wa Binadamu ya ICC. Nashangaa Watawala wenyewe Wala hata hawajali Wala kushituka kuhusiana na suala hili.

Na mbaya zaidi sana, hata Mkuu wa nchi yeye mwenyewe binafsi anakiri hadharani kwa kutoa hotuba ambazo zinaunga mkono moja kwa moja uhalifu huo. Kitendo hicho ni kujenga Ushahidi na Uthibitisho strong kabisa usioacha hata chembe ya shaka ya kuweza kuthibitisha Ukweli kuhusu kuhusika na Uhalifu huo endapo kama Kesi ya Jinai itafunguliwa kwenye Mahakama hiyo ya ICC. Mkuu wa nchi yeye mwenyewe anajitengenezea Ushahidi wa kuhusika na uhalifu huo mbele ya Mahakama ya ICC. Hotuba mbaya Sana na chafu wanazotoa hadharani zipo zinabaki kama kumbukumbu za kudumu kwenye mitandao. Mitandao inatunza kumbukumbu hizo za hotuba zao wanazotoa za "watovu wa adabu "

ANGALIZO KUBWA SANA ni kwamba, endapo kama Mahakama ya ICC itatoa Arrest Warrant ya Kimataifa dhidi ya Watawala wetu, basi Watawala hao wasije wakalalanika kwamba Mahakama hiyo ya ICC inawalenga Viongozi wa Serikali wa kutoka katika nchi za kiAfrika tu peke yake. UHALIFU mbaya na Makosa yao binafsi daima huwa ndio chanzo kikuu Cha Watawala wa nchi za kiAfrika kulengwa zaidi na Mahakama hiyo ya ICC-The Hague.
 
Back
Top Bottom