Mwanaisha Ulenge: Sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi italeta maadili katika matumizi ya teknolojia ya habari

Mwanaisha Ulenge: Sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi italeta maadili katika matumizi ya teknolojia ya habari

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1667317526778.png

Mbunge wa viti maalumu wa CCM, Mwanaisha Ulenge akichangia hoja yake katika mjadala wa Muswada wa ulinzi wa taarifa binafsi ameweka bayana kuwa sheria hii imekuja kwa wakati sahihi na inakidhi maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa sasa na wakati ujao.

Aidha, akifafanua zaidi, Mwanaisha Ulenge ameeleza kuwa ukiangalia vizuri vipengele vilivyopo katika muswaada wa ulinzi wa data binafsi utabaini kuwa umelenga kuleta maadili katika matumizi ya teknolojia ya habari.

Mwananisha Ulenge anasema katika ibara ya tano ya muswada huu imezungumzia kuhusu usafirishaji wa taarifa binafsi. Suala la usafirishaji wa taarifa binafsi linaweza kufanywa na mtu mwenyewe katika mitandao ya kijamii wanapoingiza taarifa kwenye akaunti zao. Hauna uhakika kwamba taarifa hizo unazoziingiza makampuni husika yatazitumiaje.

Makampuni mengi nchini kwetu yana saver ambazo zimehifadhiwa katika mataifa yaliyoendela hivyo hata taarifa za watu zinazochukuliwa zinahifadhiwa katika saver hizo.

Sheria hii imembana mkusanyaji taarifa kuhakikisha kwamba anatengeneza sera kamilifu zitakazolinda usalama wa taarifa binafsi. Akienda kununua saver popote anaponunua taifa hili lituhakikishie kwamba data hizo zotakazohifadhiwa ndani au nje zitaendelea kulinda usalama wa taifa letu.

Anaongeza kuwa, katika Muswada huu kuna haki ya kusahaulika kwa maana ya kwamba data zangu zilizokuwa zinatumika kwenye kampuni fulani ikitokea nimefariki natakiwa nipate haki ya kusahaulika baada ya muda fulani. Ukiangalia sheria ya uhujumu uchumiinazungumza kwamba mtu anasahaulika baada ya miaka 10, Sheria ya kodi miaka 7, TCRA miaka 5 lakini nisipotumia laini yangu kwa miezi mitatu unasahaulika.

Mwanaisha anashauri kuwa sheria hii iweke usawa kila mahali ili kuwe kuwa muda sawa wa mtu fulani kusahaulika.
 
Back
Top Bottom