Mwanajeshi amuua Kasisi aliyetembea na mke wake

Mwanajeshi amuua Kasisi aliyetembea na mke wake

Somebody sleeping in my bed, dru hill waliimba. Kifinyo kiendelee kutolewa kwa wale wote wanaodowea penzi la wenzao. Vitendo vya kula wake za watu vimezidi sana
 
Kha! Sasa baadala ya kumuua mke yeye anaua mwanaume mwenzie....jinga kabisa.
Anyways, mbususu hizi tuna share jameni tusiwe na wivu nazo
 
hata kama mwanamke atakuhakikishia vipi kwamba amemshika mumewe usiende kwake kumtafunia kwake.
Hata km akikwambia hajaolewa usiende kwake asije akakutegeshea kifiro kitakatifu ndugu yangu mpeleke unapopajua wewe unspotted by anyone usithubutu kwenda kwake hata km amekwambia hana Mume usiende kwake usipende Kitonga utakufa na kisu kikiwa kwenye njia ya haja kubwa
 
Makasisi kwa kuwa wana pesa poa za sadaka wana tabia ya kuwapeleka wake za watu katika mahotei makubwa ambapo mwenye mke hawezi kufika.
 
Mwana kulifind mwana kuliget

Nasimama na soldier. Mwanamke achepuke awezavyo ila si ndani kwangu, tena kitandani kwangu!
Hili ni darasa kubwa humu jf mchepuko unakuja ndani ya nyumba Tena anaambiwa asikutwe anakuja jf kuomba ushauri
 
  • Thanks
Reactions: I M
Kama wana watoto,, lazima mmoja wa kasisi.
 
GK5nXK8WIAENKrh.jpeg

Humu tuu
 
Hawa makasisi wa zama hizi sijui wamepatwa na nini wallah! Kila siku ni visa vyao tu mara huyu kashiriki kuua albino mara mwingine anamkula mke wa mtu! Hivi hawa watumishi siku wakikutana na Yesu watamwambiaje?
 
Hawa makasisi wa zama hizi sijui wamepatwa na nini wallah! Kila siku ni visa vyao tu mara huyu kashiriki kuua albino mara mwingine anamkula mke wa mtu! Hivi hawa watumishi siku wakikutana na Yesu watamwambiaje?
Hii dini ipigwe marufuku Tanzania
 
Soulja boy atakuwa anafeel good mno muda huu, maana kautetea uanaume wake
 
Hali ya simanzi imetanda katika kijiji kimoja huko Kapsabet kaunti ya Nandi Nchini Kenya baada ya Mwanajeshi wa Kikosi cha Ulinzi cha Kenya (KDF) kumkata sehemu za siri kisha kumuua Kasisi wa Kanisa la ACK baada ya kumfumania akifanya mapenzi na Mkewe juu ya kitanda cha Mwanajeshi huyo.

Askari huyo alipewa taarifa za siri na Wasamaria wema kuhusu Mkewe ambaye ni Mama Mshirika na pia ni Kiongozi wa Kanisa hilo kuchepuka na Kasisi huyo aliyetambulishwa kwa jina Rev Kime ndipo alipoamua kumvizia nyumbani kwake ambapo alirejea nyumbani kimyakimya usiku bila kumpa taarifa Mkewe na akaingia katika chumba kimoja bila ya Mkewe kujua ili kuthibitisha taarifa hizo.

Baada ya muda kidogo akaingia chumbani kwake na kumfumania Mtumishi huyo wa Mungu mwenye umri wa miaka 43 katika kitanda chake na Mke wake ndipo alipochukua uamuzi wa kumchoma na kitu chenye ncha kali mgongoni na kumkata sehemu zake za siri na kisha Askari huyo akatoweka kusikojulikana na Mkewe ambaye amejeruhiwa hajulikani alipo.

Majirani wameuambia mtandao wa The Star kuwa kabla ya kumuua Mchepuko wa Mkewe, Askari huyo alimfunga Mkewe kwenye kona ya nyumba ili amshuhudie wakati akimuua Mchepuko wake huyo ambapo ripoti zinasema Kasisi huyo alikuwa akisafiri KM 30 hadi kwa Mwanamke huyo na kufanya nae ngono pale Mumewe anapokuwa kwenye kazi zake za ulinzi wa Nchi.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nandi Dickens Njogu amesema “Ilikuwa tu asubuhi ya leo wakati Mkuu wa Kanisa kuu la St. Barnabas Mchungaji Nillah Bassy alipotoa ripoti rasmi ya tukio hilo la kusikitisha sana ambalo Maafisa wa Polisi walikwenda kushuhudia”

Ripoti zimesema baada ya tukio hilo Majirani walimpeleka Mchungaji huyo Rev Kemei katika Hospitali ya Kapsabet Level 5 akiwa katika hali ya umahututi na baadaye alipelekwa Eldoret na kisha akapelekwa Hospitali ya Top Hill ambako alifia akiendelea na matibabu.

Millard Ayo
Safi sana
 
Back
Top Bottom