KERO Mwanajeshi mstaafu afunga barabara ya mtaa akidai ni kiwanja chake

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hiyo ndio lugha ya kibabe inayotumiwa na wanasiasa na watumishi wa Serikali, sheria mbona iko wazi tu kuwa pale Serikali inapotaka kutwaa ardhi kwa ajili ya maendeleo, inawajibika kumlipa fidia inayolingana na thamani, kwa ukamilufu babu au bibi mwenye eneo lake analopaswa kuliachia... Sio janja janja ya kupima miguu ambayo ndio ulaghai halisi wa Serikali za mitaa.
 
Sasa hivi kila mtu ni kambale na sharubu zake
 
Hii ndio awamu ya hovyo kutokea kuliko kipindi chochote tangu tanganyika tupate uhuru. Watekaji, wauaji na mafisadi wako n mguvu kuliko mamlaka ya juu.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Inavyonekana eneo mbele hapo aliacha kwa ajili ya hizo frem...
Sijajua nini kimetokea...
Kaona hakuna biashara au!?
 
Wanasema ni komandoo.kamwambia mwenyekiti akimwondoa atakinukisha nchi nzima inuke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…