Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Erik Prince, afisa wa zamani wa Jeshi la Wanamaji la Marekani na mwanzilishi wa kampuni ya binafsi ya kijeshi ya 'Blackwater', hivi karibuni alitoa maoni yake kwamba nchi za Kiafrika zinapaswa kurudishwa kwenye ukoloni kwa sababu viongozi wake wana ufisadi na ubinafsi.
Prince alitoa mtazamo huu katika klipu fupi iliyochapishwa kwenye mtandao wa X na ‘Africa Facts Zone,’ akipendekeza kwamba ikiwa mataifa ya Afrika yanashindwa kujitawala, ni wakati wao kuvamiwa tena.
"Ni wakati wetu wa kurudisha kofia ya kifalme na kusema tutatawala hizo nchi ikiwa hazina uwezo wa kujitawala... Unaweza kusema Afrika nzima hawana uwezo wa kujitawala na kunufaisha raia wao kwa sababu viongozi wa serikali zao wanapora mali na kuziweka kwenye mifuko yao kisha wanakwenda kufanya manunuzi (kula bata) katika mji wa Paris, nchini Ufaransa badala kusaidia raia wake" Erik Prince Alisema.
Kwa mtu kama Erik Prince ambaye amewahi kuhudumu katika nafasi ya juu ya jeshi la wanamaji nchini Marekani na kuwa mwanzilishi wa kampuni binafsi ya kijeshi (Blackwater) kuzungumza kauli kama hii inaweza kuwa tishio kwa serikali za Afrika na raia wake hata kama alipitiwa katika mazungumzo.
Licha ya nchi za Afrika kuwa na mapungufu yake kama ilivyo kwa nchi zingine duniani haitoi uhalali kwa nchi za magharibi kurudisha ukoloni wao katika bara hilo kwani ni kinyume na mkataba ulioazimiwa mwaka 1960 na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu kuondoa ukoloni na kuziacha nchi zote duniani kujitawala na kuwa wamiliki halali wa maliasili zao.
Nini maoni yako kuhusu kauli ya Erik Prince?