Dogoli kinyamkela
JF-Expert Member
- Nov 21, 2024
- 618
- 1,440
Mwanajeshi wa Marine (USA) aliamua kuacha kazi jeshini na kuanza kazi mpya kama mwalimu wa high school, sasa kabla mwaka wa masomo haujaanza aliumia mgongo na akatakiwa avae plaster cast(piopi zile wanazovaa waliovunjika), akafungwa plaster cast iliyozunguka sehemu ya juu ya mwili wake kuzunguka mgongo na kifua, luckily ile cast ikakaa vizuri sana akivaa shati huwezi kugundua.
Siku yake ya kwanza akapangiwa kufundisha darasa lenye wanafunzi watukutu shuleni(na akajua kuwa kapangiwa wanafunzi watukutu), hawa wanafunzi wakajua mwalimu wao mpya ni mwanajeshi wa zamani wa marine (askari waliofundishwa kupigana kwenye maji na nchi kavu), kwakua ni watukutu wakamsubiri kwa hamu ili wamzingue waone atawafanya nini.
Wakajikusanya darasani kumsubiri kwa hamu, kama kawaida askari unatakiwa ujiongeze, akaingia darasani akakutana na kelele na vurugu za ajabu (akagundua wanampima) moja kwa moja akaenda kufungua dirisha moja la darasa hadi mwisho bila kuongea na mtu akavuta kiti akaa, sudden upepo mkali ukaanza kuingia kupitia dirishani tai yake ikaanza kupepea, muda huohuo kwa utulivu akavuta stapler (mashine yenye pini za kubania karatasi) , akashika stapler na tai yake inayopepea akatafakari kama sekunde kadhaa namna gani aizuie isipepee alafu akaigongea pini juu ya kifua chake pini ikatoboa tai na kifua, na akarudisha stapler mezani kama hakijatokea kitu.
Baada ya wanafunzi kuona tukio hilo la kutisha ghafla wote wakakaa kimya (completely quiet)
Since then wanafunzi walimpa heshima bila jamaa kusema neno hata moja na mwaka mzima wa masomo uliisha salama.