Mwanajf, Naibu Waziri, Ahudhuria Birthday Wema Sepetu, Mlimani City, Avalia Gauni la Rangi ya Chanikiwiti, Apendeza!, Atokelezea!

Mwanajf, Naibu Waziri, Ahudhuria Birthday Wema Sepetu, Mlimani City, Avalia Gauni la Rangi ya Chanikiwiti, Apendeza!, Atokelezea!

Wana Jf,
Declaration of Interest
Naomba kuanza hii thread kwa kukiri kuwa "the most powerful person on earth is a woman!", hata Adam, aliyefinywagwa na Mungu mwenyewe, akaambiwa na Mungu mwenyewe, "hiki usifanye", "usile tunda la mti wa katikati" "ukila utakufa!", lakini Adamu alipokuja kushawishiwa na mwanamke Eva, tule!, Adam alikula, na wote wakaangamia!. Hakuna any man strong enough anayeweza kushinda "the strength of a woman".

Hata mtu aliyeelezwa kuwa na nguvu kuliko binadamu wote aliitwa Samson, Nate na miguvu take yote was nothing mbele ya mwanamke mrembo Delilah, hivyo na mimi naomba kukiri kuwa, hata mimi, mbele ya wanawake, niko very weak, hivyo leo nimejikuta nalazimishwa kuangalia Wasafi TV, live ikonyesha birthday ya mnyange mlimbwende Wema Sepetu, ikitangazwa live kutoka Mlimani City, na nimelazimishwa kuangalia by non other than a woman!, kiukweli wanawake wana power na command!.

Hivyo katika kufuatilia sherehe hiyo, ndipo nikamuona mwana jf mwenzetu, ambaye ni Naibu Waziri akitinga kwenye red carpet, na kiukweli ametokelezea kwa kupendezea na gauni lake la rangi ya Chanikiwiti.

Jee kuna ubaya wowote, kumsifia mwana jf mwenzetu, ukimuona mahali ametokea na ametokelezea?.

Macho yameona, nimeamua kukiri amependezea!, hongera mwana jf mwenzetu na hilo gauni lako la Chanikiwiti.

Naomba msiniulize ni nani na wala msiulizie picha, wewe jua tuu ni mwana jf mwenzetu ambaye ni naibu waziri, amehudhuria hafla birthday ya mnyange mlimbwende Wema Sepetu.

Nawatakia furahi DEI njema

P.
We nawe....[emoji850]
 
Back
Top Bottom