MwanaKJJ Jumatano: Jaji Kaijage Anapata Shida Kusimamia Uchaguzi TZ?

Au ile ya "wapigwe tu hamna namna'',ni moja kati ya kauli isiyo ya kiungwana kabisa,kwa hili inadhihirisha wazi raia hawana haki ya kupata wanachotaka mpaka Rais aamue,hili halina ubishi hata NEC na jeshi la polisi.
 
Umeniwakilisha vyema Mkuu.
 
Waweza kuwa sahihi
Nina chuki kubwa na Narcisists walioko madarakani JMT lakini zaidi sana wale ambao hujitoa akili kuwasifia machizi hao
Wewe ni mmoja wao
Nakuchukia sana

Chuki inakuangamiza wewe mwenyewe; so jitahidi ujiponye. Ila kama inakufanya ujisikie vizuri keep it.
 

Why don't they quit? Hili ndio jambo sitaki kusikia watu wanalitetea.. wewe mtu mzima, umesoma, una gololi zako mbili bado unafanya kazi kwa kuogopa kwani ni lazima uwe na nafasi hiyo? Mbona watu wengi wanaishi tu nje ya serikali?
 
Mkubwa hakosei ila umempaka mafuta kwa mgongo wa chupa naamini atakuelewa
 
NDUGU MEXENE MELLO et al.,
Naomba mnipige ban ya miaka miwili mpaka 2020.siwezi kuendelea kusoma maoni ya / comment ya wana Lumumba wapumbafu na machoko.
Ila endeleeni kushangilia, wakati bado unakuja .Magufuri kaweka vyombo vya habari kwapani, mahakama kwapani, jeshi la polisi kwani, bunge kwapani,shughuli za kisiasa na democrasia kwapani, taasisi za kidini kwapani nadhani uchunguzi kakobe mmeusikia. Shangilieni ,imbeni mtakavyo weza, tukaneni vyama pinzani mtakavyo weza, nunueni madiwani na wabunge mtakavyo weza ,ueni upinzani kadiri nguvu zenu zitakavyo weza.Ule mwisho badoo, Magufuri akianza kuuwa watu wake ndani ya ccm akihisi wanamuhujumu na wengine ndani ya chama chake , ndipo ule wakati uliotabiriwa utakuwa umewadia. Mtatafuta pa kukimbilia mtakosa, mtalia na kusaga meno ,mtaomboleza lakini hamtaona msaada wala hakuta kuwa na kimbilio. Endeleeni kushangilia, endeleeni kusifia.....siku zaja.
 
Upuuzi huyo. Keenge tu kama ndugu yake. Analipwa kujinyeeea.
 
Why don't they quit? Hili ndio jambo sitaki kusikia watu wanalitetea.. wewe mtu mzima, umesoma, una gololi zako mbili bado unafanya kazi kwa kuogopa kwani ni lazima uwe na nafasi hiyo? Mbona watu wengi wanaishi tu nje ya serikali?
Mzee MWANAKIJIJI hapa umepotoka, mamlaka ya Rais nafikiri unayafahamu vizuri sana, changanya na uafrica wetu sasa
 
Au ile ya v"wapigwe tu hamna namna'',ni moja kati ya kauli isiyo ya kiungwana kabisa,kwa hili inadhihirisha wazi raia hawana haki ya kupata wanachotaka mpaka Rais aamue,hili halina ubishi hata NEC na jeshi la polisi.
Hapana, hilo nalikumbuka sawa sawa na lilitoka kwa Mzee Pinda! Ninalosema mimi lilitoka kwa Mkulu mwenyewe siku Lowassa alipozungumzia Masheikh wanaoshikiliwa kule Zanzibar!

Mkulu akaunganisha hilo pamoja na la Kibiti na kuchomokea suala la Manji "kukamatwa na sare za JWTZ" huku Mkulu akitoa kauli ya kuashiria sare hizo za kijeshi huenda zina connection na mauaji ya kule Kibiti (Manji ana jeshi; au?).

Mwisho wa yote Mkulu akatoa kauli kuashiria atashangaa endapo Jeshi la Polisi halitamkamata na kumhoji mtu "hatari" kama Lowassa!

Ile kauli yangu ya kwamba nimesahau kidogo ni mbwembwe tu za uandishi lakini nakumbuka vyema kauli kadhaa za Mkulu zinazoashiria kuagiza Jeshi la Polisi kushughulikia watu badala ya issue ingawaje Mzee Mwanakijiji haoni ni namna gani Rais anaweza kuhusishwa moja kwa moja na yanayoendelea huku akijitia uziwi kusikia kauli mbalimbali za Rais zinazo-encourage watendaji wa serikali kuenenda in unprofession way!

MM wala haoni ni namna gani wala hailekei kwamba Rais anakerwa na mambo ya hovyo yanayofanywa na watendaji wa serikali na taasisi zake!

MM anajitia kutojua kwamba kwa mambo kadhaa yaliyotokea nchi hii, Rais alitakiwa awe ameshamfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani! Na kwavile Rais hajafanya na wala haielekei kwamba atafanya hivyo; bado MM anajitia kutojua kwamba kwa kutochukua hatua, basi yote hayo ni kama yanaungwa mkono na Rais lakini hata kama anaunga mkono bado ni dhambi kumuhusisha Mheshimiwa Mkuu!

Na kama tunataka kumuhusisha rais; according to MM's new arguing style; tunatakiwa ku-justify in one way or another kwamba ingawaje yanatokea under Mkulu's nose; hayo si mapya kupata kutokea duniani let alone Tanzania!

Kwamba; yalipata kutokea enzi za akina Chief Mangungo, yakatokea enzi za Mwarabu! Yalitokea enzi za Mjerumani na Mwingereza! Yakatokea enzi za Mwalimu, Mwinyi, Mkapa na Kikwete!

Kwahiyo tusimsimange Mkulu kwa mambo yaliyopata kutokea hata mbele ya macho ya mitume!
 
 
Huyu mzee nilikuwa namheshim sana lakini nini sijui kilimkuta mzee naomba rudisha akili yako ya zamani
 
Hivi waliojiandikisha kupiga kura walikuwa wangapi, na waliopiga kura walikuwa wangapi? Je tunaolalamika tulikuwa miongoni mwa wapiga kura?
only a fool will think this way

kwamba tusijadili kisa hatukupiga kura
 
Nimesoma makala hii kutoka kwa nguli na mwanafalsafa wa JF, ndugu Mzee Mwanakijiji na hakika nimebaki kuwa puzzled na mashaka makubwa. Mara nyingi topic za namna hii huwa napita kimya kwa sababu wengi ya wachangiaji ni sehemu ya tatizo la mfumo wa nchi hii..! Lakini kabla sijaendelea, nilijiuliza yafuatayo;-
  1. Je mwandishi anajua anachokisema?
  2. Je mwandishi alishindwaje kutofautisha kati ya mfumo/system, udikiteta, Democrasia and Illiteracy?
  3. Is he biased?
  4. Je mwandishi huyu ni zao la kodi ya wananchi?..etc
  5. Je hawa ndo aina ya political analyst wa Nchi hii?
Ndugu mwandishi ukipata muda njoo ujibu maswali/ hypothesis hapo juu ili tuwekane sawa. baada ya kusema hayo, naomba nijikite kwenye hoja kama ifuatavyo;-

Mosi, mwandishi hayuko focused. ameshindwa kueleweka anatetea nini, kwa manufaa ya nani na kwa ajili gani. truth be told, hii article tungeipeleka kwa serious editors...Isingeliona jua! Nilitarajia mwandishi achambue tatizo la mfumo (system) na jinsi yanayotokea kwa sasa kuwa ndo engineering ya mfumo wenyewe. Mfumo wa siasa wa Tanzania goes back to history wakati wa Nyalali commission kuhusu siasa za vyama vingi. Report inaonyesha about 80% walipinga kuwepo kwa vyama vingi...huku asilimia 20% tu ikikubali uwepo wa multiparty system in Tanzania. Hii inamaanisha nini? It means, bado watu hawana elimu ya kutosha kuhusu democrasia na uwepo vyama vingi nchini. Such illiteracy bado iko kubwa miongoni mwa viongozi wa serikali including RAIS na Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. with such analysis, ndo maana tunaona chuki, uonevu, mauaji dhidi ya wapinzani..

The Political Parties Act [CAP 258 R.E. 20024, Ibara ya 4(1) inasema kuwa Kutakuwa na Msajili wa Vyama vya Siasa katika ofisi ya Waziri Mkuu au katika ofisi nyingine kama Rais anavyoweza kuamua na atachaguliwa na Rais.There shall be a Registrar of Political Parties in the office of the Prime Minister or in such other office as the President may determine who shall be appointed by the President.Hali kadhalika, sheria ya tume ya uchaguzi inasema katika ibara ya 6(1) kuwa There shall be a Director of
Elections who shall be appointed by the President from amongst the names of senior civil servants of the United Republic recommended by the Commission.

as i quote you...Jaji Kaijage Anapata Shida Kusimamia Uchaguzi tz? The answer is yes! kwa sababu zifuatazo;-

  1. Is biased, kwa kuwa ni mteule wa Rais
  2. Hayuko independent kwa sababu iliyoainishwa hapo juu
  3. Is Illiterate kwa sababu ni sehemu ya ile 80% percent ya Nyalali Commission
  4. Ni mwanachama wa CCM...(I have evidence)
Rule against biases: Mwandishi yuko biased. I quote..."Wapo wanaosema naogopa kumnyoshea kidole Rais Magufuli kwa sababu nilimuunga mkono kugombea kwake kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015. Inachonishangaza ni kuwa hata watu wanaojua uandishi wangu wanafikiria kwa sababu fulani sijajiunga kwenye jukwaa la wanaotaka watafute uhalali wao wa kisiasa kwa kuonesha wanampinga Magufuli". Kwa Introduction ya namna hii, umekosa credibility ya kuendelea kufanya submission na kuna-invalidate article nzima na kuwa redundant. labda nikuulize swali, whom are you fighting with?

Mwalimu Nyerere akiwahutubia ma-judge wa kipindi hicho huko tabora, aliwahi kusema kuwa "Mahakama zetu katika kila ngazi lazima ziwe huru na mkono wa mtendaji wa serikali (executives). Uhuru wa kweli unahitaji kwamba raia yeyote anajiamini kuwa kesi yake haitakuwa na uamuzi wa upendeleo, hata kama ni kesi dhidi ya waziri mkuu."....Je msajili yuko huru? je mahakama ziko huru? Free from whom?...Maybe from executives?...probably yes..probably no!

Issue nyingine yenye ukakasi ni pale mwandishi aliposema kuhusu as i quote..."Jeshi la Polisi. Sijasema tatizo ni Askari Polisi". Nijuavyo mimi askari polisi ni sehemu ya jeshi la polisi na hawatenganishiki.

HENCEFORTH, one may conclude that;-

  1. Article yako haina mashiko
  2. You lack skills on analyzing political issues
  3. Hauko focused
  4. Hukufanya Research wakati unaandiika article hii
Cheers, Prof
 
Mkuu maisha magumu sana,
Hata huko Marekani na Nchi zilizo endelea ukiona yeyote anajiuzulu jua ana uhakika na maisha yake kiusalama na kiuchumi.

Sasa nitajiuzulu vipi nikiwa sina uhakuka na ugali wa kesho??
 
w
WEWE NI MNAFIKI TU HATA UJIFANYE KUFUMBA MACHO, ULISHASIKIA TANGAZO TANGAZO KUWA MKURUGENZI NAMLIPA MSHAHARA, NAMPA GARI NA NYUMBA LEO ATANGAZE WA UPINZANI??????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????? HALAFU LEO UNAJICHETUA UONEKANE UNASIMAMA UPANDE WA HAKI. MFYUUUUUUUUUUUUUUUUUUU
 
Yaani kuna watu mpka unatamani uwe unakutana nao nje y jf mzungumze mawili matatu.
Uchambuzi mzuri. Hongera profesa. Unautendea haki "uprofesa".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…