Mwanamageuzi mkongwe wa Urusi Chubais ajiuzulu kama balozi wa Putin

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Pamoja na kukwama kwa wanajeshi wa Urusi kusonga mbele vitani nchini Ukraine , Rais Putin anaonekana amepata pigo kutoka ndani ya Kremlin yenyewe.

Mmoja wa washauri wake, Anatoly Chubais, amejiuzulu kutoka jukumu lake kama mjumbe wa kimataifa - afisa mkuu zaidi kujiuzulu tangu kuanzishwa kwa uvamizi.

Ripoti za Urusi zilisema kwa sasa yuko Uturuki na mkewe
Bw Chubais alipewa kazi ya kuratibu malengo ya maendeleo endelevu ya Urusi kimataifa.

Baada ya vita kuanza alichapisha picha ya kiongozi wa upinzani aliyeuawa, katika kile kilichoonekana kama ishara mbaya.

Hakukuwa na maoni yoyote ya kuandamana na picha yake ya Facebook ya Boris Nemtsov, katika kumbukumbu ya kuuawa kwake kwa mtazamo wa Kremlin. Pia hajatoa maoni yoyote kuhusu kujiuzulu kwake.

Chanzo kimoja kililiambia shirika la habari la Tass kuwa ameondoka Urusi na pia kujiuzulu uwakilishi maalum wa Rais Putin.

"Ndiyo, Chubais amejiuzulu kwa hiari yake mwenyewe. Lakini ikiwa ameondoka [Urusi] au amebaki, hilo ni jambo lake binafsi," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema.

BBC Swahili
 
Sijui wananchi wa Russia wanaishije sasa kiuchumi. Ni dhahiri Ukrain ipo hovyo ila kwa Russia sina uhakika.

Hii ya leo inaondoa morale ya kupambana kwa askari pamoja na raia pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani mshauri aondoe morali ya wanajeshi kupambana amekuwa mkuu WA majeshi ivi nyie mnakuwaga na akili kweli au mmesomea chini ya miti
 
kitu

anachokifanya Putin kwa mbeleni kina manufaa sana kwa taifa lake ila kwa kuwa kila kitu lazima kiwe na upinzania ni lazima wengine wasimame wazungumze. kila mtu anaelewa umuhimu wa taifa kuwa kitu kmoja na kulinda mipaka yake anachofanya putin ni kulinda taifa lake dhidi ya mataifa ya nje na pia muendolezo wa taifa lake. Hiyo ndo maana wanajeshi wako kwa ajili ya kulinda mipaka na kutetea taifa lake
 
No reason justifies invasion and killing of innocent people!
 
Mkuu ukweli hakuna mwenye haki juu ya uhai wa mwenzake . ila hizi silaha zinatengenezwa na binadam dhidi ya binadamu wengine, Haya mataifa tunayoishi yamejengwa kwa jasho na damu hivyo watu wanatumia jasho na damu kulinda haya yote.fikiria raisi wa ukraine angelisema tokea mwanzo kuwa taifa lake halitajiunga na nato je haya yangetokea.
No reason justifies invasion and killing of innocent peopl
 
Pamoja na kukwama kwa wanajeshi wa Urusi kusonga mbele vitani nchini Ukraine , Rais Putin anaonekana amepata pigo kutoka ndani ya Kremlin yenyewe.

Mmoja wa washauri wake, Anatoly Chubais, amejiuzulu kutoka jukumu lake kama mjumbe wa kimataifa - afisa mkuu zaidi kujiuzulu tangu kuanzishwa kwa uvamizi.

Ripoti za Urusi zilisema kwa sasa yuko Uturuki na mkewe
Bw Chubais alipewa kazi ya kuratibu malengo ya maendeleo endelevu ya Urusi kimataifa.

Baada ya vita kuanza alichapisha picha ya kiongozi wa upinzani aliyeuawa, katika kile kilichoonekana kama ishara mbaya.

Hakukuwa na maoni yoyote ya kuandamana na picha yake ya Facebook ya Boris Nemtsov, katika kumbukumbu ya kuuawa kwake kwa mtazamo wa Kremlin. Pia hajatoa maoni yoyote kuhusu kujiuzulu kwake.

Chanzo kimoja kililiambia shirika la habari la Tass kuwa ameondoka Urusi na pia kujiuzulu uwakilishi maalum wa Rais Putin.

"Ndiyo, Chubais amejiuzulu kwa hiari yake mwenyewe. Lakini ikiwa ameondoka [Urusi] au amebaki, hilo ni jambo lake binafsi," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema.

BBC Swahili
Putin akimkamata atamweka kizuizini .
 
ha ha ha ha.naona marekani ameona atokee plan B ,kuwahonga midola mabarozi ili wajihuzuru .Na huyo harudi Russia ,Sana Sana ataenda marekani kuanza maisha ya mapya ya ubilionaire wa pesa ya kuhongwa na USA.
 
Mkuu ukweli hakuna mwenye haki juu ya uhai wa mwenzake . ila hizi silaha zinatengenezwa na binadam dhidi ya binadamu wengine, Haya mataifa tunayoishi yamejengwa kwa jasho na damu hivyo watu wanatumia jasho na damu kulinda haya yote.fikiria raisi wa ukraine angelisema tokea mwanzo kuwa taifa lake halitajiunga na nato je haya yangetokea.
Ni kivipi nchi inayojitawala ifanye maamuzi kwa matakwa ya nchi nyingine, wewe ungekubali kutojiunga na taasisi unayoona itafaidisha nchi yako kisa nchi nyingine inakuambia usijiunge?
 
Huyo ameona hawezi kufanya kazi na mtu fyatu ndio akaamua kusepa kwani anaona jinsi nchi inavyozama na kutengwa na dunia ya wastaarabu.
 
Yani mshauri aondoe morali ya wanajeshi kupambana amekuwa mkuu WA majeshi ivi nyie mnakuwaga na akili kweli au mmesomea chini ya miti
Huna unachojua, kwanza ungetaka kujua kwann kajiuzulu na maana yake ni nini?

Hali ya rusia ukraine haiendi vizuri putini na aila zake walikurupuka miscalculated, jana jeshi lao limerudishwa nyuma 100 kilometers ni strong organised Ukrenian defence
 
kitu

anachokifanya Putin kwa mbeleni kina manufaa sana kwa taifa lake ila kwa kuwa kila kitu lazima kiwe na upinzania ni lazima wengine wasimame wazungumze. kila mtu anaelewa umuhimu wa taifa kuwa kitu kmoja na kulinda mipaka yake anachofanya putin ni kulinda taifa lake dhidi ya mataifa ya nje na pia muendolezo wa taifa lake. Hiyo ndo maana wanajeshi wako kwa ajili ya kulinda mipaka na kutetea taifa lake
Unalindaje mipaka ya taifa lako kwa kuvamia nchi nyingine?!
Kumbuka Ukraine ni taifa huru kama Tanzania ilivyo. Ni Sawa Sawa na Uganda ivamie hapa kwetu kwa kisingizio cha kulinda mipaka yake
 
Back
Top Bottom