Mwanamalundi wa Kisukuma

Mwanamalundi wa Kisukuma

Jamaa alikuwa na mambo mengi sana, Wajerumani walikuwa wanamshika na kumuweka ndani ila wakifunga wakiondoka wanamkuta hayupo tayari yuko nje na mambo yake, kwa story ni kwamba alikuwa na uwezo wa kutembea juu ya maji. Pia kuna sehem kuna alama zake za makalio alikaa kwenye jiwe alivyotaka akaacha alama za makalio kwenye jiwe. Pia kwenye mawe maarufu ya Mwanza Bismark Rock jamaa alizamisha nondo kuzunguka jiwe kwa mikono yake tu hadi leo nondo zipo kwenye hayo mawe.
 
Jina lake Halisi aliitwa Igulu Bugomola
Mzaliwa wa Nela, kwa sasa ni wilaya ya Kwimba, mkoa wa Mwanza.
Alikuwa mtukutu sana enzi za utoto wake na alikuwa na miguu mirefu sana. Alipenda kucheza ngoma hivyo alienda sehemu nyingi kushindana. Kutokana ma utundu wake wa kurubuni watoto wengi kwenda kwenye ngoma na kuacha kujishughulisha kwenye shughuli za kilimo na mifugo, watu wengi walimtukana huku wakimwambia “lilolagi lya mamilundi malihu lilibahumbula abiye”kwa tafsiri ya kiswahili “lione na miguu yake mirefu linarubuni webzake” na ikapelekea mpka hilo jina kuitwa ng’wanamalundi.

Ushindi katika mashindano ya ngoma katika jamii za usukumani huhusishwa na ushirikina na hivyo kufanya wacheza ngoma wengi kutafuta dawa kwa waganga wa kienyeji. Katika harakati za kutafuta dawa hizo za kushindana kwenye ngoma ndipo alijikuta ameangukia kwenye kupata uwezo wa hiyo miujiza mikubwa iliyonfanya awe mtu maarufu kuwahi kutokea katika jamii ya kisukuma.

Aliibuka mshindi mara zote katika ngoma na kuwashinda manguli kama Gindu nkima (mghani na bingwa wa mbina ya wigashe) pamoja na Samike ambaye naye alikuwa mcheza ngoma maarufu. Aliwaonyesha miujiza wajerumani walipomkata kwa sababu ya kukwamisha shughuli za ujenzi wa reli ya kwenda Mwanza. Mwanamalundi aliyekamatwa pamoja na wenzake ambao ni Mtemi Makongoro wa Ilemela na Kaliyaya aliyekuwa mwanasiasa ambaye alipinga mambo mengi ya wajerumani. Mwanamalundi na mtemi Makongoro walitoka kwa miujiza kwenye mikono ya wajerumani lakini Kaliyaya aliishia kunyongwa. Mwanamalundi alifanya miujiza mingi ikiwemo kuvuka bahari, kusonta mimea na watu vikakauka na baada ya kuzikwa mvua ilinyesha kwenye kaburi lake tu.

Kumekuwepo na watu wengi wenye miujiza tangu zamani za Mwanamalundi, kabla na baada yake kama vile Mbusule (mtabiri), Gindu Nkima (Mghani na mcheza ngoma), Mtemi Makongoro Igana, Samike, Kaliyaya (mwanasiasa) na wengine lakini Mwanamalumdi amekuwa kinara wao.
Sababu ya kufa yeye ilikua ni nini
 
. Mwanamalundi alifanya miujiza mingi ikiwemo kuvuka bahari,
1695420883079.png
 
Back
Top Bottom