Mnapokubaliana kufunga ndoa, maana yake ni kwamba kuna makubaliano ya kimkakati kuhusiana na maisha yenu mmejadiliana na kukubaliana. Kubwa moja wapo ni kuhusiana na ajira na kipato.
Changamoto huja; Mmoja anapobadilika katikati ya safari ya ndoa, mfano (hauhusiani na Flavy) tunakubaliana lets say utafanya mambo ya urembo hapa US kwa 90% inayobaki utafanyia kwingine na mimi shughuli zangu zitakuwa hapa hapa ili tupate kuijenga na kuiimarisha ndoa yetu.
Baada ya ndoa unabadilika, 95% shughuli zako unafanyia nje ya US, jukumu la ndoa linakuwa si kipaumbele tena. Lazima mgogoro uanze. Na hii inareflect pande zote kike na kiume!!
Kikubwa si kufanana, unapooa au kuolewa maana yake umeongeza jukumu!! Lile jukumu unaloongeza utalimudu? Utalilea? Na makubaliano mnayokubaliana utakwenda nayo maisha yenu yote? Amini nakuambia, ukikubaliana na mwenzio na mkaenda sawa. Ndoa hudumu, ila ukibadilika tu! Umeharibu!!
Vijana wengi siku hizi hubadilika, bint mmoja alikuwa maarufu kipindi cha nyuma kidogo. Jamaa kaoa, wamekubaliana wakaishi Arusha, binti katulia tuliii ndoa inakwenda na anafanya biashara zingine kabisa tena kwa mafanikio.