Mwanamke adai DNA imevunja ndoa yake

Mwanamke adai DNA imevunja ndoa yake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
aliyeachika.jpg
Frederica Michael,mwanamke anayelalamikia kipimo cha DNA.

KWA UFUPI
‘Nilimpenda mno mume wangu Mushi, Mungu anajua, lakini ameniacha kwa sababu ya majibu ya
DNA ambayo nina hakika yalifanyiwa hujuma au yalikosewa katika mikono ya binadamu," alisema mwanamke huyo kwa uchungu.

MWANAMKE mmoja mkazi Ilala, ameibuka na kukishutumu kipimo cha vinasaba
(DNA) cha kutambua uhalali wa baba kwa mtoto, kwamba hakina ukweli kwani kimevunja ndoa yake.

Frederica Michael, aliyefika ofisi za gazeti hili jana, alikosoa kipimo hicho kuwa kina upungufu mkubwa, kwani hakikutoa majibu ya ukweli katika kesi ya uhalali wa mtoto wake mwaka 2005.
Alisema mwaka 2005, familia hiyo ilikwenda kupima kujua iwapo mtoto wao aliyezaliwa mwaka 2004, ni mtoto halali wa mume wake, Constatine Moshi.

"Nimejifungua Aprili 11, 2004 wakati huo mume wangu alikuwa safarini, aliporudi na kumkuta mtoto alibadilika na kusema siyo wake," alisema Michael.

Alisema mume wake alikuwa akimtuhumu kuwa, ana uhusiano na bosi wake jambo ambalo mwanamke huyo alilikanusha vikali.

Wiki hii gazeti hili lilitoa takwimu za mwaka huu za matokeo ya vipimo vya
DNA kutoka maabara ya Mkemia Mkuu, ambazo zinaonyesha asilimia 44 ya waliokwenda kupima uhalali wa baba siyo wazazi halisi wa watoto hao.

Mwanamke huyo alisema mume wake, alimkataa mtoto huyo akidai ana asili ya Kiarabu jambo ambalo Michael alilikataa na kudai kuwa, ukoo wao ni weupe na wana nywele laini hivyo yawezekana amerithi upande huo.
Alisema mgogoro huo ulikua na mwaka 2005, waliamua kupima
DNA na Julai 20, mwaka huo huo majibu yalitoka yakionyesha mtoto huyo siyo halali wa Constatine.
Michael anakanusha vikali majibu hayo, akisema yana upungufu mkubwa kwani yeye ndiye anayeujua ukweli.

"Sikuwahi kuzini nje ya ndoa tangu nimefunga ndoa mwaka 1999 na mume wangu Mushi ambaye nimezaa naye watoto saba," alisema.

Alisema kipimo hicho kinatekelezwa na wanadamu, hivyo wanaweza kufanya makosa ambayo yameigharimu ndoa yake.
‘Nilimpenda mno mume wangu Mushi, Mungu anajua, lakini ameniacha kwa sababu ya majibu ya
DNA ambayo nina hakika yalifanyiwa hujuma au yalikosewa katika mikono ya binadamu," alisema mwanamke huyo kwa uchungu.

Alisema ni vyema
DNA kitumike kwa uangalifu kwani kinaweza kusababisha migogoro zaidi katika jamii.

Hata hivyo, Mkemia Mwandamizi wa Kitengo cha Masuala ya Jinai, Baiolojia na
DNA, Gloria Machuve alisema kipimo hicho ni sahihi na kinatoa matokeo yenye ukweli kwa asilimia 99.
Machuve alisema maabara hiyo ilinunua mitambo bora zaidi na kisasa, ili kupata matokeo yenye uhakika hivyo matokeo yake yana uhakika na ukweli. Mwanamke adai DNA imevunja ndoa yake - Kitaifa - mwananchi.co.tz

WABONGO JIHADHARINI NA MAMBO YA KUPIGA DNA MTAKUJA KUHARIBU NDOA ZENU KAMA UNAMPENDA MKE WAKO NA UNAMUAMINI USIPIGE DNA TAFADHALI UTAKUJA KUHARIBU NDOA YAKO BORA UKUBALI YAISHE TU USIMCHUNGUZE KUKU ANAKULA NINI UTASHINDWA KUMLA SHAURI YENU WABONGO MCHANGA WAPWANI HUO MIMI SIMO.



 
duu,halafu wana watoto7,huyo baba anatafuta sababu tu
Bibie kisukari inaonyesha huyu Mzee mwenye huyu mke amesha choka kulea watoto sio wake ingelifaa awapime wote hawa watoto saba DNA na akigunduwa wote sio wake atachukuwa uamuzi gani? Bibie kisukari hujambo lakini?
 
BAK, naomba kwanza kibao cha bushoke 'mume bweg@' kiniburudishe wknd ya leo. Manake mtoto katoka mwarabu kumbe karithi kwa bibi.
Yaani tatizo huwa linaanzia kwenye accusations za usaliti. Mwanaume ambae out of nowhere atadai dna test ndo tutamshangaa, lakini kama mgogoro wa uaminifu ulikuwepo kabla, dna demand sio cha ajabu. Sasa dna test ni bure mama, karudie.
 
Last edited by a moderator:
Nyinyi wanawake muna tuonea sana sisi waume zenu,unakuwa na mume ndani ya ndoa huku pembeni una Bwana wa Siri ahhhh What is this?
 
duu,halafu wana watoto7,huyo baba anatafuta sababu tu

aafu ndoa wamefunga 1999, loh! Au walishaanza kabla? Ila haya mambo za kuzaa mtoto wa kiarabu na kudai kwenu weupe hapana. Weupe wa kiafrika hautoi mwarabu!
 
Back
Top Bottom