Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
4.Mtoto wa mama:
Inawezekana mwanaume akalazimika kuishi nyumbani kwao kwa muda baada ya kumaliza masomo au amepoteza ajira na akawa bado hajapata ajira au hajapata shughuli ya maana itakayomwezesha kujitegemea, hii inakubalika. Hata hivyo kama mwanamke anakutana na mwanaume ambaye anaishi na wazazi wake na haonyeshi dalili za kutafuta kazi au shughuli yenye kipato itakayomwezesha kuondoka hapo kwao na kujitegemea, usije ukajiingiza katika uhusiano na mwanaume wa aina hiyo, itakula kwako, huyo ashakuwa kupe na tegemezi, utakuwa ni mzigo wako na atakuganda kama luba na kupoteza bahati ya kukutana na wanaume wenye mwelekeo wa maisha.
Mtambuzi
Aisee hapa umenigusa nimechoka kukaa home saaaana.. na hata demu wangu nimeachana nae na sitaki tena demu mpaka niondoke home...