Mwanamke akipendeza anamfurahisha nani?

Mwanamke akipendeza anamfurahisha nani?

Hili nalo wazo kama kuna mawazo chanya kwa huyo mume! Kuna wengine hawapendi mke/mpenzi aonekana mtanashati kwa watu.. na hivyo hujitahidi sana kuficha wasipendeze kwa hofu ya kitu fulani.

Hujasikia wanaume wengine wakikataza wake zao kutengezea nywele, kuvaa mitindo fulani n.k? Sasa huku ndio kukosa confidence kwa mkatazaji maana hajiamini kuwa ni yeye tu!
Ila mwisho wa siku pamoja na kupendeza lazima staha/heshima nayo iwepo na siyo kuvaa mivalio yenye kukutia aibu wewe na wale walio karibu nawe.

WOS,

Kama unagundua baadaye kuwa Mr hana confidence unafanyaje? Utaamua kumbuluza tu na yeye anyamaze?

Nashauri ukigundua hivyo tena ukiwa umechelewa ama uteme mzigo au ukubali kuishi na hicho kilema.
 
DC
Uzuri haya mambo hayaji ghafla. Huja taratibu..na hapo utakuwa na muda wa kuamua unyoe au usuke! Kama mchumba kila mara hana confidence... utakuja kulia ukishakuwa wife!
 
kumbe hii ni kwa wanandoa tu....DC mi sikujua bana!!

i will consider my hubby ntakapofunga ndoa......

for now najikonsider mwenyewe

Bht,

Kama bado upo upo tutakuongelea ili iweje? Wewe ni full kujiachia. Na kama jamaa anaanza kuingiza timu wakati huo anakuja na masharti hata ukitema mzigo poa tu. Ila hukumu ikishapita (kama ilivyomtokea mshikaji - G ) basi hapo huna ujanja!
 
Mnapokuwa wawili - mke na mume au wapenzi kuna kitu kinaitwa maridhiano katika mapenzi.Hata mimi kuna wakati naweza kumpa Mr ujiko wa kunichagulia anavyotaka nivae tunapoenda matembezi ya pamoja.. au nikishavaa namuuliza umependa? akisema hapana ..nitabadili hadi aridhike maana nimempa uhuru wa kunichagulia siku hiyo....
na yeye hufanya hivyo hivyo.Ukiangalia scenerio hizi ni tofauti na hii tuliyowekewa hapa tujadili.Hapa hatuangalii kwenda kuwapendezesha watu wa nje bali sisi wenyewe wahusika.

Mtu mzima awe mwanamke au mwanaume anatkiwa awe na uhuru mradi haupelekei kuvunja amani au heshima.
 
Well said WoS. mi wa kwangu napenaga apendeze hata kama sipo,, Niajiamini.
 
Mnapokuwa wawili - mke na mume au wapenzi kuna kitu kinaitwa maridhiano katika mapenzi.Hata mimi kuna wakati naweza kumpa Mr ujiko wa kunichagulia anavyotaka nivae tunapoenda matembezi ya pamoja.. au nikishavaa namuuliza umependa? akisema hapana ..nitabadili hadi aridhike maana nimempa uhuru wa kunichagulia siku hiyo....
na yeye hufanya hivyo hivyo.Ukiangalia scenerio hizi ni tofauti na hii tuliyowekewa hapa tujadili.Hapa hatuangalii kwenda kuwapendezesha watu wa nje bali sisi wenyewe wahusika.

Mtu mzima awe mwanamke au mwanaume anatkiwa awe na uhuru mradi haupelekei kuvunja amani au heshima.

Umemaliza kila kitu. Ngoja nikatafute lunch. Mkishakuwa wawili siyo mmoja tena na lazima kutakuwa na mambo mengi ambayo huwezi kupata au kufanya kila kitu kama ulivyopenda 100%. Kwangu mimi huo ndio msingi wa kila kitu tunachofanya leo na hata tutakachofanya kesho n.k.
 
Mimi huwa napendeza kwa faida zangu binafsi,wala si kwaajili ya kumfurahisha mtu.
 
si ndio sucrifices hizo kwenye ndoa!!!!
kila mmoja lazima kuna vijimambo ataviacha ili amridhishe mwenzake!!
 
Weekend hii nilimpitia mshikaji wangu mmoja pamoja na rafiki yake wa kike ili twende kwenye party. Nilipofika nilikuta mtafaruku fulani kuhusu nguo gani avae shemeji. Mshikaji alimng'ang'ania shemeji avae nguo ndefu wakati shemeji alin'ga'ngania anataka avae nguo fupi. Huyo mshikaji akawa anamwambia unataka kumfurahisha nani huko na dada akajibu "naipenda tu nguo hii na nikivaa nahisi kupendeza. Kwa hiyo nafurahia mwenywe wala simfurahishi mtu kama unavyodhani". Mshikaji wangu alisisitiza kwamba yeye ndo alitakiwa afurahishwe.

Baada ya kuwasihi kwa muda walielewana, shemeji akatinga kivazi kirefu na tukaenda zetu kula raha.

Tukio hili linikumbusha rafiki yangu mmoja ambaye mke wake aligombana na mama mkwe wake kwa kumzuia kuvaa nguo fupi. Mke alisisitiza kuwa kwa kuwa mume wake anaridhika yeye haoni tatizo.

Hivi, mwanamke anapojipigilia pamba akapendeza lengo linakuwa ni kuifurahisha nafsi yake, au kumfurahisha ampendaye, kuwafurahisha walimwengu au kuwaonyeshea wanawake wenzake?

hapa hata mimi niko gizani maana mamaa hapa huwa tukiwa na mtoko wiki nzima anahangaika avae nini ili apendeze zaidi,yaani atafanya hata shoping tena wakati nguo ndani zipo za kutosha kabisa na bado hata akinunua hizo mpya anaweza asizivae vilevile kwa kutoridhika nazo,na mimi huwa akiniuliza namwambia aah hapo umependeza,akiuliza tena namwambia eeh umependeza sana akiuliza tena najibu ndio hizo zimekupendeza zaidi,najibu tu almradi aridhike asisumbue na yeye kashashtuka sasa anasema we muongo unasifia tu almradi,hapo nashindwa kuwaelewa wanawake.
 
Mimi huwa napendeza kwa faida zangu binafsi,wala si kwaajili ya kumfurahisha mtu.

May be hata huyo mtu wa kumfurahisha huna.

Amini usiamini, ni raha sana kusikia mwenzio amefurahishwa na jinsi ulivyotoka.
 
hapa hata mimi niko gizani maana mamaa hapa huwa tukiwa na mtoko wiki nzima anahangaika avae nini ili apendeze zaidi,yaani atafanya hata shoping tena wakati nguo ndani zipo za kutosha kabisa na bado hata akinunua hizo mpya anaweza asizivae vilevile kwa kutoridhika nazo,na mimi huwa akiniuliza namwambia aah hapo umependeza,akiuliza tena namwambia eeh umependeza sana akiuliza tena najibu ndio hizo zimekupendeza zaidi,najibu tu almradi aridhike asisumbue na yeye kashashtuka sasa anasema we muongo unasifia tu almradi,hapo nashindwa kuwaelewa wanawake.

Wakati mwingine inatokea na hasa hasa kama muda umeenda sana na mnachelewa ila hicho ni kitu kibaya sana kwani humtendei haki. Akipata shiga yake akamtoa kasoro anaweza kukuchukia. Mimi huwa najitahidi kumweleza ukweli.
 
Mwanamke kiumbe cha ajabu.
Saikolojia inasema mwanamke anafanya mambo kushindana na mwanamke mwenzake.
Kuhusu mavazi ni hivyo hivyo.
My take-anatakiwa kushirikiana na mumewe/mpenzi wake kuhusu aina gani ya mavazi avaie.ie anatakiwa amfurahishe mumewe na mwanamme amfurahishe mkewe.
 
Wakati mwingine inatokea na hasa hasa kama muda umeenda sana na mnachelewa ila hicho ni kitu kibaya sana kwani humtendei haki. Akipata shiga yake akamtoa kasoro anaweza kukuchukia. Mimi huwa najitahidi kumweleza ukweli.
mara nyingi anakua kashapendeza lakini hajiamini,hata nikimweleza ukweli sometime yeye anakua hajaipenda hiyo nguo,ndio maana mwisho nachoka naamua kuitikia tu vyovyote maana mie huwa sioni mantiki yoyote apendeze sana asipendeze kwangu doesnt matter.
 
Shurti mwanamke apendeze na sio kumpendezesha mume, mashoga nk, yeye mwenyewe nafsi yake!
 
Weekend hii nilimpitia mshikaji wangu mmoja pamoja na rafiki yake wa kike ili twende kwenye party. Nilipofika nilikuta mtafaruku fulani kuhusu nguo gani avae shemeji. Mshikaji alimng'ang'ania shemeji avae nguo ndefu wakati shemeji alin'ga'ngania anataka avae nguo fupi. Huyo mshikaji akawa anamwambia unataka kumfurahisha nani huko na dada akajibu "naipenda tu nguo hii na nikivaa nahisi kupendeza. Kwa hiyo nafurahia mwenywe wala simfurahishi mtu kama unavyodhani". Mshikaji wangu alisisitiza kwamba yeye ndo alitakiwa afurahishwe.

Baada ya kuwasihi kwa muda walielewana, shemeji akatinga kivazi kirefu na tukaenda zetu kula raha.

Tukio hili linikumbusha rafiki yangu mmoja ambaye mke wake aligombana na mama mkwe wake kwa kumzuia kuvaa nguo fupi. Mke alisisitiza kuwa kwa kuwa mume wake anaridhika yeye haoni tatizo.

Hivi, mwanamke anapojipigilia pamba akapendeza lengo linakuwa ni kuifurahisha nafsi yake, au kumfurahisha ampendaye, kuwafurahisha walimwengu au kuwaonyeshea wanawake wenzake?

Binadamu yeyote yule awe mwanamke au mwanaume anapoamua kuvaa nguo huwa anafanya hivyo kutokana na hisia alizonazo kwamba nguo ile inampendeza zaidi na humpa raha ndani ya roho yake kwa kujua kwamba amependeza.

Na kwa maoni yangu ni kosa kubwa kwa mwanaume kumlazimisha mkewe/GF avae nguo anayoitaka yeye badala ya ile anayoitaka mkewe/GF wake. Kama hili hii linatokea basi ili kuepusha ugomvi ni bora tu kukubaliana na uamuzi wa mwenzio kuhusu ni nguo gani anayoitaka kuivaa badala ya kumlazimisha avae nguo asiyoitaka.
 
Mnapokuwa wawili - mke na mume au wapenzi kuna kitu kinaitwa maridhiano katika mapenzi.Hata mimi kuna wakati naweza kumpa Mr ujiko wa kunichagulia anavyotaka nivae tunapoenda matembezi ya pamoja.. au nikishavaa namuuliza umependa? akisema hapana ..nitabadili hadi aridhike maana nimempa uhuru wa kunichagulia siku hiyo....
na yeye hufanya hivyo hivyo.Ukiangalia scenerio hizi ni tofauti na hii tuliyowekewa hapa tujadili.Hapa hatuangalii kwenda kuwapendezesha watu wa nje bali sisi wenyewe wahusika.

Mtu mzima awe mwanamke au mwanaume anatkiwa awe na uhuru mradi haupelekei kuvunja amani au heshima.

umeelezea vizuri sana WOS,
mrs wangu huwa anapenda kunipachagulia nivae nini,lkn kwa sababu nguo zote nilizonazo nazipenda huwa hainipi shida namkubalia,kazi ni anaponiambia nimchagulie yeye,to be honest i dont have a taste na women clothes apart from jeans na tops au mini na top.....kwahiyo huwa nakuwa diplomatic namwambia kila anachovaa huwa anatoka bomba,naogopa kum-disappoint
 
Back
Top Bottom