SoC02 Mwanamke aliye bora kwa mumewe anatakiwa awe na sifa gani?

SoC02 Mwanamke aliye bora kwa mumewe anatakiwa awe na sifa gani?

Stories of Change - 2022 Competition

Nasibu hemedi

Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
11
Reaction score
4
Kwa majina naitwwa Ramadhani Selemani Ramadhani ni kijana wa Kitanzania leo ningependa kuzungumzia sifa za mwanamke alio bora kwa mumewe.

Wote tunafahamu kuwa duniani kila kiumbe hai mungu amekiumba katika jinsia mbili ambayo ni jinsia ya kike na jinsia ya kiume. Ninapozungumzia mwanamke bora kwa mumewe ni yule mwanamke alio olewa yani yupo katika ndoa yake bila hujali ana watoto au bado hajafanikiwa kuwa na watoto.

Kipindi cha nyuma au katika dini zetu baadhi zilokuwa zinakataza mwanamke kuwa mtafutaji wa familia mfano mwanamke kufanya biashara yoyote ilikuwa hairuhusiwi na badala yake alikuwa anaandaliwa kuwa mama wa nyumbani tu basi.

Kwa upande mwingine walikuwa sahihi kwa kipindi hicho ila kwa kipindi hichi cha utandawazi tunaona wanawake na wanaume wakifanya kazi katika nyanja mbalimbali mfano waalimu, madokta, mpaka wengine kuwa maraisi.

Mwanamke kwa nafasi yake na asili ya mwanamke ni mwangalizi wa familia yani baba na watoto kama watakuwepo kwa wakati huo hatakama huyo mwanamke ni mfanyakazi wa serikalini au ni mjasiria mali. Katika familia baba anajukumu la kuhakikisha familia inapata maitaji ya msingi kama vile chakula mavazi na malazi bila kujali kipato chake.


Je, Mwanamke alio bora kwa mumewe anatakiwa kuwa na sifa zipi?

(a) Awe na huruma na mumewe; hii ni sifa ya msingi sana ya kugundua je mke ulie nae ni mwanamke bora na sahihi kwako. Mwanamke asipo kuwa na hiruma basi utayaona maisha machungu hatakama utakuwa na kipato kikubwa hutaona raha ya maisha.

(b) Mwanamke bora lazima awe mvumilivu; kwenye maisha kuna kupata na kukosa kwahio mwanamke lazima awe mvumilivu na lazima akubali kuwa kuna kupata na kukosa sio siku mumewe amkekosa na yeye anaondoka na kumkasirikia mumewe.

(c) Mwanamke bora kwa mumewe lazima awe mnyenyekevu mbele ya mumewe; kuna baadhi ya wanawake wanajisahau sana na kujiona wao wapo juu zaidi bila kujua sifa ya mwanamke hata kidini haruhusiwi kuwa juu ya mwanamume hata kama mumewe hana kipato chochote. Unakuta mwanamke anapaza sauti kwa mumewe bila kujali ni mazingira gani waliopo.

(d) Mwanamke bora kwa mumewe lazima amsikilize mumewe palee anapoambiwa jambo lolote lile; kuna baadhi ua wanawake wanakuwa wakaidi sana kwa wanaume zao mfano mume anakuambia tulia usitoke hapa nyumbani bila ruhusa yangu basi mwanamke yulee hukaidi na kuondoka bila ruhusa ya mumewe. Kama mwanamke atakuwa na tabia hii basi kila siku ndoa nyingi zitakufa na zitakuwa na migogoro isio kuwa na lazima.

(b) Mwanamke bora kwa mumewe lazima apende familia na ndugu kwa ujumla haijalishi ni ndugu zake au ndugu wa mumewe kwa sababu kama atakuwa hapendi ndugu zake au ndugu wa mume ni kiashiria huyo mwanamke ni mbinafsi hana ushirikiano na wengine.

Je, ni tabia gani mwanamke aliyepo katika ndoa akifanya huharibu ndoa yake?

(a) Kuwa na mahusiano mengine ndani ya ndoa yake. Hii huvunja ndoa kwa ssbabu kwa asilimia kubwa mwanamke anapokuwa na mahusiani na mwanaume mwingine anaanza dharau kwa mume wake bila kujua kuwa mwanaume hata awe maskina hataki kuzarauliwa.

(b) Mwanamke kutoa siri za mumeo nje; mwanamke hatakiwi kumwaga ya ndani kwake kwa mtu yoyote hata awe mzazi wake hapaswi kutoa siri njee kwakuwa utakapo fanya hivyo basi mumeo akifahamu atakosa uaminifu katika ndoa yake.

(c) Mwanamke kukosa heshima na kujisitiri; hakuna mwanaume anaependa kuona mkewake anakosa stara kwakuwa mwanamke asipo jieshimu na kujositiri huleta picha mbaya kwa jamii na watoto pia.

Mwanamke akiona mumewe amekosea inatakiwa amuambie kwa utaratibu mzuri na mwanaume anatakiwa aelewe sio kwakuwa yeye ni mwanaume akiambiwa anabisha hii sio nzuri na itamfanya mkeo asiwe huru kukuambia unapo kosea tena.

Mwanamke ukiona mumeo kafanya kosa usiogope kumuambia badala yake na wewe unafanya kosa ili wote muwe sawa hapo wote munakosea na munaweza pelekea kuharibu ndoa yenu kwa pamoja

Mwanamke unatakiwa utambue mwanaume ni kama mtoto wako wa kwanza katika maisha yako hawezi kukushinda kwakua mwanaume kwa mke ni kama mtoto hana ujanja hivyo kuna viti mwanaume anaitaji kwa mkewe.

Mambo hayo ni kama yafuatavyo:

(a) Mwanaume anaitaji kudekezwa.
(b) Mwanaume anaitaji kuthaminiwa.
(c) Mwanaume anaitaji kupendwa kwa dhati yani kwa shida na taabu na raha.

Je, Mwanamke atakupenda ukiwa hutimizi majukumu yako.

Jibu ni sio kweli ili mwanamke akupende lazima mwanaume utimize majukumu yako na umuoneshe upendo wa dhati sio yeyetu akuoneshe upendo wewe hujali hapo hatakupenda kabisa na hamtaishi kwa raha kwenye ndoa yenu.

Watu wengi wanaamini ukiwa na pesa ndio unapendwa na unaishi vizuri na mke au mume ila mimi nasema sio kweli wengine wanapesa na hawapendwi na hawana furaha katika ndoa zao japo pesa ni muhimu kwa ajili ya maitaji ila sio kigezo kikubwa cha kufanya upate furaha ndani ya ndoa. Wapo watu masikini sana na wanaishi kwa furaha na amani kuliko wenye pesa.

Madhara ya kuowa mwanamke asio jitambua.
(a) kuongezeka kwa watoto wa mtaani; hii hutokana na ndoa nyingi kuvunjika haliakuwa wengine wamesha zaa watoto na kupelekea watoto kutanga tanga mtaani na kukosa hakizao za msingi.

(b) ongezeko la maradhi mfano UKIMWI; hii hutokea kwakuwa unaowa mwanamke hajitambui anakuwa sio mwaminifu kwenye ndoa yake anakuwa na mahusiano zaidi ya mumewe mwisho hupata marazi na kuleta ndani.

Kwa pamoja mwanamke na mwanaume inatakiwa tupendane na tujaliane ili kujenga familia bora na kupata vijana walio na tabia njema kwa faida ta taifa la kesho.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom