Mwanamke amuua shemejiye baada ya kumpiga kofi makalioni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Polisi eneo la Suna Magharibi, kaunti ya Migori wanamsaka mwanamke mwenye umri wa makamo aliyetoweka baada ya kumdunga kisu shemejiye.

Eunice Adhiambo alitekeleza kisa hicho baada ya mabishano makali kuzuka baina yake na shemejiye mnamo Jumanne, Disemba 24.

Mwanamke ammua shemejiye kwa kumzaba kofi kwenye makalio yake.

Kulingana na chifu wa eneo hilo Yogo Tumbo, marehemu alikuwa amemtembelea mshukiwa ambaye alimkuta akichonga mihogo kulingana na ripoti ya Citizen TV.

Inadaiwa, jamaa aliyejaribu kujadiliana kuhusu jambo fulani ambalo bado halijajulikana alimzaba kofi Eunice katika makalio yake baada ya kuhisi mshukiwa alikuwa akimpuuza.

Mwili wa mwenda zake unahifadhiwa katika makafani ya hospitali ya Migori Level Four ukisubiri upasuaji. Picha: Citizen TV.

Punde si punde, mshukiwa anadaiwa kumrukia marehemu na kumdunga mara kadhaa kifuani akitumia kisu alichokuwa nacho mkononi.

Chifu huyo alidokeza kwamba, mwenda zake alifariki papo hapo na mwili wake unahifadhiwa katika makafani ya hospitali ya Migori Level Four ukisubiri upasuaji.
 


miss zomboko makafani maana yake ni nini? Hicho ni kiswahili?
 
Nilikuja speed nikajua marehemu kafa kwa kupigwa kofi la makalioni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…