Pre GE2025 Mwanamke anahaki ya kuongoza taifa hili. Watu waelewe nchi yetu haiongozwi na Dini wala Mila na desturi bali Katiba ya Nchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu naona juzi umetekenywa kidogo kuhusu kupata nafasi ya uandishi huko juu, naona unajaribu kuimpress mamlaka za uteuzi kwa post za kichawa. Sio vibaya kiutaftaji, lakini ni kama umeshoboka kirahisi mno😂

Ningekuwa natafuta teuzi ningekuwa nishapata Mkûu.

Nazungumzia uhalisia wa mambo
 
Kûna clip naziona mtandaoni zinasambaa zinazojaribu kueleza kuwa mwanamke hatakiwi KUONGOZA lakini wanashindwa kumalizia kuwa hapaswi KUONGOZA katika muktadha wa Kidini tenà Dini Fulani. Au Mila na desturi Fulani
Hakuna chochote wanachoweza kufanya hata kama dini fulani au mila fulani haziruhusu.
 
Kwahiyo unabishana na aliyoyaamrisha ALLAH (S.A.W) ? Wewe kama nani?

Mwanamke hajaumbwa kumuongoza Mwanaume, hivyo ndivyo Quran aliyoshishiwa Mtume Muhammad (Rehma zimfikie) itakavyo
 
Kwahiyo unabishana na aliyoyaamrisha ALLAH (S.A.W) ? Wewe kama nani?

Mwanamke hajaumwa kumuongoza Mwanaume, hivyo ndivyo Quran aliyoshishiwa Mtume Muhammad (Rehma zimfikie) itakavyo

Allah sio mungu wa Watañzania ila wàpo baadhi ya watañzania wanamuamini.
 
Tusipangiane, kila mtu abaki na mtazamo wake. Mimi kwetu ujaluoni ni never ever mwanamke kuwa kiongozi. Nitaheshimu na kufuata sheria kama taratibu ambazo tumekubaliana nchi iongozwe lakini haimaanishi ya kwamba mtazamo wangu utabadilishwa na izo sheria.
 

Hakuna nchi ya wajaluo Wala Taífa la wajaluo.

Rais anayeongoza nchi wanaoishi wajaluo wa Tanzania ni Mwanamke au Mwanaume?
Spika wa Bunge àmbalo wajaluo wanaishi Tanzania ni Mwanaume au mwanamke?

Hiyo Never yako uliyoitaja ni kuridhisha Nafsi yako au kukataa uhalisia?

Kama wewe ni mjaluo lakini Rais wako ni Mwanamke tenà àmbaye siô mjaluo hiyo inakupa pîcha gàni akilini mwako??
 
Adui wa Mwanamke NI Mwanamke mwenzake

Kipi kwako ni chakike, Motherboard au Nafsi yako?
Maana unaumia na kuona wivu kusikia Wanawake wakitetewa.
Hapana sisikii wivu wala kuumia ila napinga ujinga unaoendekeza.
Unawadanganya hawa mabinti, acha tuwaambie ukweli

1) Singo maza.
2) Uongozi kwa mwanamke.

Unaposema katiba haijamkataza Mwanamke, kwani wapi imemtaja mwanaume?(mambo mengine hutatuliwa kwa utashi tu, na kwa utashi wa kawaida, Mwanamke hawezi kuwa kiongozi)
 
Kweli Kwa wanaoamini hivyo lakini siô kweli Kwa wanaoamini katika mîungu Wengine na sio kweli Kwa wasioamini katika mîungu.

Ndîo maana serikali haina Dini maana ikileta Dini patakuwa na machafuko
Serikali ya Tanzania ina Dini mbili Uislam na Ukristo,ndio maana huwa inaomba wazi kwa Imani hizo mbili

Ndio maana pia inawatambua na kuwaalika mara kwa mara viongozi wa Dini hizo Ikulu na katika mikutano mbalimbali

Kusema Serikali haina dini ni Uongo
 
Sio tuu hakuna mambo ya Mila Wala dini zao kwenye Katiba pia hatuna Ardhi za kimila ,Kila mtu ana Haki na usawa Kwa vyote bila kujali Jinsia yake 👇👇
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…