Mwanamke anayejiweza kimaisha

  • Thread starter Thread starter JS
  • Start date Start date
Ushauri mdogo kwa anayetaka kumwoa mwanamke mwenye uwezo
1. Usiishi kwenye nyumba yake, ikibidi kama anayo mpangishie mtu na nyie mkapange sehemu nyingine.
2. Usiajiriwe kwenye shughuli za mkeo, tafauta ajira au biashara zako mwenyewe
3. Usiache dini au dhehebu lako na kuhamia la mkeo, yeye ndio akufuate mnakosali
Ukitimiza hayo matatu utaishi maisha ya furaha LAKINI ikifanye tofauti utaishi maisha ya huzumu sana maishani mwako. Hivi kama unaishi kwenye nyumba ya mkeo, mama mkwe wako au shemeji zake wakija hapo nyumbani unafikiri wanakuona kama mkwe wao au kigaragosi fulani?

Ushauri wa mwisho shikamana na mnaendana naye kiuchumia ili mjijenge pamoja kwani unayemkuta na mali pengine amenunuliwa na mwanaume mwenzio na LAZIMA aendelee kulipa fadhila pindi nafasi inapopatikana au hata kumzalia humo humo kwenye ndoa yako
 
Ngoja mdogo wetu Teamo aje atueleze. Kwamba kwenye briefcase anazo zaidi ya 100m za EPA halafu anaburuzwa ki-Bushoke Bushoke tena bila kupigwa shuntama (Limbwata)i!!
unajua mkulu hoja hapa iko hivi....
kwamba Re: Mwanamke anayejiweza kimaisha

kwamba huyu mwanamama ndo baasi tena KUOLEWA?....
lakini hoja ya senti roya kwamba uwe na hela AGAIN UWE WEAK!hiyo mi sikubali!kwasababu katika hali ya kawaida kabisa hiyo haiwezi kuwa ndoa wala mapenzi
 

Hivi bado mnabishana tu?

We bana kama unataka mambo yako yakuendee hovyo we kajiolee mwanamke aliyekuzidi kipato, elimu na/au umri. Hii ni kwa Mujibu wa uzoefu, hakuna cha findings, journals wala scientific proof hapo.

Haya hebu twendeni kule tukapige kampeni Chat Room irudishwe.:fencing:
 

:fencing:
 

Teamo, hilo do lilikuwa swali la JS. Na jibu tumempatia kuwa ni "BIG NO"


Mkuu, you got it wrong. Kwa hiyo toa jibu sasa kama swali umelielewa!:eyeroll2:
 
Teamo, hilo do lilikuwa swali la JS. Na jibu tumempatia kuwa ni "BIG NO"



Mkuu, you got it wrong. Kwa hiyo toa jibu sasa kama swali umelielewa!:eyeroll2:
mkuu mimi naona kama sijakosea kabisa tafsiri........!
 

Hapana ndugu yangu sikupindisha ukweli bali nilikuwa najaribu kufafanua kutokana na mchango wa NN aliposema kwamba inabidi mwanamke aache kila kitu ili amridhishe mume. ikumbukwe kwamba mwanamke huyo anayejiweza inawezekana kabisa hali hiyo inasababishwa na ajira yake ambayo ana kipato kikubwa kutokana na nafasi aliyonayo kwa muajiriwa wake ambayo ameipata kutokana na kiwango cha juu cha elimu aliyokuwa nayo.
 

NN ulichoandika hapo ni kweli kabisa. Nimeyaona matukio kama hayo mara nyingi sana katika ndoa zetu za Kitanzania. Mke anapokuwa na elimu au kipato kikubwa basi inawezekana kabisa kikawa chanzo cha kukosa amani ndani ya nyumba na hatimaye hata kuivunja ndoa.

Hmmmm, " si unajiona unapesa ndio maana unafanya hivyo" au umejiona umekuwa manager ndio mie sifai tena" mafanikio yako badala ya mwenzio kuyafurahia yanakuwa karaha karibu kila siku iendayo kwa Mungu.

Kitu kidogo tu basi utaambiwa umefanya hivyo kwa sababu unamuona njemba hafai una kipato kikubwa na umekuwa meneja sasa au mkurugenzi na blah blah blah chungu nzima. Mahusiano haya jamani yana matatizo kweli kweli.

YouTube - ‪Nu Shooz - Point Of No Return 1986‬‎
 
We bana kama unataka mambo yako yakuendee hovyo we kajiolee mwanamke aliyekuzidi kipato, elimu na/au umri. Hii ni kwa Mujibu wa uzoefu, hakuna cha findings, journals wala scientific proof hapo.:

Hapo tupo pamoja watu wanapumulia mashine kwa kuoa watu wa design hii.
 

DC, hapa chini ni link ya kile ya kuthibitisha kile nilichoandika kwamba Wanawake ambao ni mama wa nyumbani na si waajiriwa wanakuwa na mahusiano zaidi ya nje, lakini katika hii article wanachukuwa namba ya pili baada ya Walimu na hii ni US sijui kama kutakuwa na tofauti kubwa kama utafanywa utafiti kama huu Tanzania.

Doctors, Stay-At-Home Moms Likely To Cheat: Survey
 
Are you kidding me?? This is unbelievable.:shocked::shocked::shocked::shocked::shocked::shocked::shocked::shocked::shocked::shocked::shocked:
 
Hebu nipe contacts zake ASAP.
:ranger:
 
kwahiyo mwanamke aache kila kitu kwa ajili ya kuolewa au just to help guys with their insecurity problem?
Hell NOOOOOOOO. We kama una mshiko mbona wa kukuoa wapo wengi tu wala huachi kitu. Ila kumbuka mtii mumeo.:thumb::thumb::thumb:
 

Kwani ni uongo kama mtu amekuzidi pesa tayari you are less powerful than she/he is financially kwa hiyo siyo mwanaume anajiona bali ndiyo hali halisi hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…