Come on Dark City just loosen up a little kwa ndugu zako wa kike. Kwani miwani ya jua nayo inakuwa issue tena wajameni??
Huyo anayevaa usiku naye hayuko sawa kwa kweli.
Atatumia pesa yake kama bakora kukuadhibu na kama ndo unaishi kwake dah unakuwa mtumwa nimeshuhudia jamaa zangu
JS,
Mbona mimi napenda sana wadogo zangu wapate raha na Mungu awapatie waume wema kama mimi?. Ila miwani hiyo nayo ni tatizo.
Kama wewe una tambia njema usihofu kabisa. Ila kama na wewe umeanza kuongelea puani na tena kiswahili cha ki-Spanish basi ujue kazi unayo. Vinginevyo usiwe na shaka! Hata hivyo usithubutu ku-cross boundary eti? Maskini kwa maskini na wenye nazo wao kwa wao, sawa!!:nod::nod:
Ndio
Siyo wote Fidel labda huyo awe hana mapenzi ya dhati, wadada wengi tu pesa wanazo, kama ni kitabu kwa sana lakini bado wananyanyaswa na wanaume mpaka mtu unajiuliza ni kwanini lakini?
sio wote na wengine mnasababisha nyie, ukae kwangu nikusaidie hili na lile bado nijue unanichezea rafu...nakutimua faster.
Kweli bwana make kila kitu likitokea jambo, wanasema msubiri mama, wakati we upo! Mie siwezi hali hiyoAtatumia pesa yake kama bakora kukuadhibu na kama ndo unaishi kwake dah unakuwa mtumwa nimeshuhudia jamaa zangu
Apo mdogo wangu mwogope Mungu (japo najua huvai) lakini kweli kwenye gari kunakuwa na jua? mbona basi magari mengi yanayoendeshwa hapa sio convertibles? Mtu unakuta yupo kwanye Rav 4 ya kawaida tu or whatever, yenyewe vioo ni tinted, na mtu kavaa miwani ya jua, na pengine hata siku hiyo hakuna jua!
the other thing is hamshangai wanaume hawavai? na kwa nini iwe tu pale mtu anapopata mkoko kabla unakuta yuko kawaida tu wala havai miwani....na je daktari anakuwa amewapima jamani?
Wadada wenye pesa na hali nzuri mm nawaogopa sana.
Kuna ndugu na rafiki zangu kadhaa walibahatika kuoa wadada wa design hii leo wanalia na kusaga meno, wadada tuongee ukweli wakiwa na pesa na wakiolewa jamaa kaja kaona mafanikio kama hayo jiulize nn kitatokea kwa mdau??? Muulize Teamo na Asprin
Fidel hapo umenena.Wadada wa siku hizi hasa wenye nazo ni matatizo mtindo mmoja na wengi hawana heshima kabisa,unaweza kuwa nae kwa mapenzi yote lakini mwisho wa siku atakuja kukuumiza tu na inapofikia mkigombana ndio kabisa atakwambia uchukue time kwani hana shida na wewe ulikuwa ni mzigo kwake.
Kwanza wadada wa dizaini hii huwa ni ngumu sana kuolewa na hata kudumu katika mahusiano.
Ngaamka mshiki...Waamka Asprin????
Mimi big brother, nikiwa na akili zangu timamu, na bila ya kushauriwa wala kulazimishwa na mtu yoyote, nawashauri vijana wa kiume ambao hawajaoa kuwa wasithubutu wala kujaribu kuoa wanawake wa aina zifuatazo, kama wanataka ndoa imara:
- Waliowazidi kimapato
- Waliowazidi kielimu
- Waliowazidi kiumri.
Nimeongelea kwa uzoefu kwa hiyo sipendi kuulizwa maswali. Kama wanabisha, wajaribu halafu yakiwashinda wakuje hapa kuanzisha masredi ya kuomba maushauri ya ma griit sinkaz!