BUK, sidhani kama kuna mwanaume (kati ya wale waliotoa michango yao) amesema/kuonesha kuwa anapenda amke wake aache kazi. Hapo unajaribu kupindisha mada kuu inayojadiliwa hapa. Swali ni kuwa, mwanamke anayejiweza anapata shida kuwapata wanaume wa kumuoa? Na baadhi yetu (tena wengi tu) tumesema ndiyo na tukatoa vielelezo, ikiwemo uzoefu wetu na tafiti za kisayansi. Pia hapa hakuna suala la insecurity kama anavyosema Noname. Suala ni preferences za wanaume, na kwamba walio wengi wangependa kumuoa mwanamke asiyewazidi kipato. Maisha ya ndoa yanakuwa na furaha kama wahusika wanafurahia maisha yao na ndio maana kila jinsi (gender) inakuwa na vitu vyake inavyoviangalia na pia kila mtu anazo tastes zake.