Mwanamke au mwanaume wako akijiunga Badoo muogope

Mwanamke au mwanaume wako akijiunga Badoo muogope

Habari za muda wanajukwaa,

Niende kwenye mada moja kwa moja,

Nimekuwa nikijaribu kufanya mawasiliano na baadhi ya wanawake kwenye mtandao wa Badoo, lakini cha ajabu asilimia kubwa kama sio wote, mkishaanza mawasiliano wataanza kuomba vocha, mara nauli, mara hela ya kula, mara ya saluni, sasa najiuliza kwanini hawa wanawake wako hivyo.

Mbona wao kila ukianza kuwasiliana nao ni mizinga tu na usipowatumia, au ukiwachana wanapotea kimoja, leo nimewasiliana na wanne wapya wote wamenipiga mizinga, mmoja hela ya kula, mwingine nauli na wengine wawili hela ya saloon, kwa nini wako hivi, wakuu hebu nipeni uzoefu wenu kuhusu hawa watu.
 
maeneo ya kwenu hakuna wanawake kwani, hadi uende badoo sijui facebook wacha wakupige mizinga hakuna namna
 
Ulitaka waombe nini..!? Kaza moyo tuu tuma hizo pesa, acha uchoyo..!!

Haha haaaaaa alitaka wamuombe dusheeeeee.....
Nao wanaangaliaga mtu wa kumuomba. Mbona wanaume wengine hawaombwi ombwi hovyo hovyo
 
Njia rahisi siku izi ya kupunguza kero kwa wanawake hiyo ukijifanya unajua kutongoza tu mtandaoni unapigwa mzinga fasta hurudi tena
WANAWAKE ONGEZENI KUWAPIGA MZINGA HAWA WATONGEZEA MITANDAONI
 
Hakuna mtandao wa kishamba kama badoo.., watu wanaotumia huo mtandao hua hawaelewek eleweki, uswahili mwingi na ushamba ndo umejaa kule, kiukweli app yenyewe nime uninstall
 
Hakuna mtandao wa kishamba kama badoo.., watu wanaotumia huo mtandao hua hawaelewek eleweki, uswahili mwingi na ushamba ndo umejaa kule, kiukweli app yenyewe nime uninstall
Ushamba upi? Walioko huko wanajua wanachokifanya huko inawezekana inawanufaisha
 
hahaha yaan leo leo na mzinga wa hela ya saloon,kwan kabla yako alikua na kipara [HASHTAG]#BADOO[/HASHTAG] OYEEE#
 
Kwani badoo ndio nini maana mara ya pili naona watu wanalalamika humu hebu mnitoe ushamba
 
Hakuna mtandao wa kishamba kama badoo.., watu wanaotumia huo mtandao hua hawaelewek eleweki, uswahili mwingi na ushamba ndo umejaa kule, kiukweli app yenyewe nime uninstall
wew uliyeingia kichwa kichwa mpaka ukajitoa ndo mshamba, aya tuambie mjanja umehamia wapi IG??
 
Back
Top Bottom